

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ametoa wito kwa wafanyabiashara na taasisi za fedha kutumia fursa za miundombinu na uwepo wa makao makuu ya serikali Jijini hapo kuwekeza kwenye miradi itakayo wezesha Jiji hilo kuwa la kibiashara.
Wito huo umetolewa leo tarehe 25.05.2024 wakati wa maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa chama cha ushirika, akiba na mikopo (SACCOS) ya kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Arusha Road Jijini Dodoma .
Mhe.Senyamule amesema Jiji la hilo lina fursa mbalimbali za miundombinu ikiwemo ya barabara,reli na viwanja vya ndege ambayo ikitumika vyema na wafanyabiashara na taasisi hizo itasaidia kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
"Hadi kufikia mwakani kiwanja cha ndege msalato kitakuwa kimekamilika, hivyo tunapaswa kutumia fursa hiyo kwa kujenga hoteli za kisasa na kuangalia namna ambayo Dodoma inaweza kuwa tofauti haswa kwenye uwekezaji na biashara, tunataka Dodoma iwe kitovu cha kila kitu na haya yote yanawezekana chini ya Saccos kubwa kama KKKT Arusha Road Saccos" Ameeleza Senyamule
Ametoa shime kwa wanachama wa SACCOS hiyo kuendelea kuweka akiba pamoja na kukopa na kurejesha kwa wakati mikopo hiyo Ili kupata faida itakayowawezesha kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kijamii ikiwamo ya kurejesha uisani kwa Jamii (CSR)
Kwa upande wake Mwakilishi wa mtendaji Mkuu wa tume ya maendeleo ya ushirika (TCDC) Bw. Kisamalala Josephat amewapongeza viongozi wa Saccos hiyo kwa kufuata sheria za Ushirika ikiwemo kuwahamasisha wanachama kushirikiana na kurejesha mkopo kwa wakati.
Naye Afisa ushirika Mkuu Halmashauri jiji la Dodoma Bw.Joseph Chitinka awewashauri kutafuta watalaam watakaowasaidia kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa hoteli l, uwekezaji wa kibiashara Ili kujijenga kiuchumi.
Maadhimisho hayo yenye kaulimbiu "BORESHA MAISHA NA KKKT ARUSHA ROAD SACCOS LTD" ilitanguliwa na semina kwa wana Chama hao.
Maiko Salali Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mpwapwa, Apongeza CCM kwa Ujumuishwaji wa Makundi Maalum
DIB YAHIMIZA WANANCHI KUDAI FIDIA ZAO KUTOKA BENKI ZILIZOFILISIKA
USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA
DWIGHT DANDA KIJANA MDOGO NA MHITIMU WA CHUO KIKUU ATIA NIA UBUNGE KIBAMBA
BoT YAWATAKA TAMFI NA TAMIU KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA.
Aliyeongoza kura maoni Vunjo 2020, kumkabili tena Dkt. Kimei
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake
Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma