TAWA yapongezwa kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu ukerewe | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

TAWA yapongezwa kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu ukerewe

Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA imetoa elimu kwa wakazi wa kijiji cha Serema kata ya Bwiro wilaya Ukerewe wanaoishi pembezoni mwa ziwa Victoria lengo ikiwa ni kuwasaidia kujikinga na majanga ya uvamizi wa wanyama aina ya mamba na viboko ambao wamekuwa wakiathiri maisha ya wananchi ambao baadhi yao hupoteza uhai.

The Dododma Post
By The Dododma Post
10 May 2024
TAWA yapongezwa kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu ukerewe

Hayo yamejiri Kufuatia wakazi wa maeneo mbalimbali hapa nchi kutochukua tahadhari za mara kwa mara katika kujilinda na wanyama wakali ambao ni hatarishi kwa maisha yao.

Beatus Maganja ambae ni Afisa Habari mamlaka ya Usimamizi wanyama Pori Tanzania TAWA amewaeleza wananchi hao kuwa serikali imejipanga kikamilifu ili kuhakikisha wananchi wanakuwa salama.

"katika kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu Serikali inahakikisha usalama wa mwananchi unakuwa ni kipaumbele cha kwanza na ndiyo maana mara kwa mara Maofisa wa TAWA wamekuwepo maeneo mbalimbali nchini kutoa elimu na kufanya doria katika maeneo ambayo yanatajwa kuwa na changamoto ya wanyamapori hao". Amesema hayo Maganja.

Kwa upande Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Bw. Joshua Manumbu ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania  TAWA kwa elimu wanayoendelea kuitoa katika jamii namna ya kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyamapori wakali na waharibifu hususani mamba na viboko na kuwadhibiti pale wanapoonekana kuhatarisha maisha ya wananchi.

"Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na Maofisa wa TAWA kutoka Kanda Maalumu ya Mwanza na imetoa ushirikiano mkubwa kwa Maofisa hao ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo" .amesema hayo Manumbu

Kwa upande wao,  wananchi wa Kijiji cha Selema kilochopo Kata ya Bwiro wilayani humo wameipongeza na kuishukuru TAWA kwa elimu wanayoendelea kuitoa wilayani humo ambayo wamekiri kuwa imekuwa msaada kwao na itawawezesha  kuendelea na shughuli zao za kiuchumi huku wakiepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyamapori hao.

Mamlaka ya usimamizi wanyamapori Tanzania TAWA imekuwa ikitoa elmu maeneo mbalimbali hapa nchini lengo ikiwa ni kuwafikia wananchi wanaoishi maeneo hatarishi dhidi ya wanyama hao.

KAMATI YA  KUDUMU YA BUNGE YA  NISHATI NA MADINI YAPEWA ELIMU KUHUSU UKOKOTOAJI WA BEI ZA BIDHAA ZA MAFUTA NCHINI

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAPEWA ELIMU KUHUSU UKOKOTOAJI WA BEI ZA BIDHAA ZA MAFUTA NCHINI

RAIS DK SAMIA-BARAZA LA USALAMA NA AMANI NI NYENZO MUHIMU AFRIKA.

RAIS DK SAMIA-BARAZA LA USALAMA NA AMANI NI NYENZO MUHIMU AFRIKA.

SI MAJANGA YOTE YA MOTO MAJUMBANI YANASABABISHWA NA UMEME WA TANESCO.

SI MAJANGA YOTE YA MOTO MAJUMBANI YANASABABISHWA NA UMEME WA TANESCO.

KASEKENYA asisitiza uadilifu kwa mafundi sanifu

KASEKENYA asisitiza uadilifu kwa mafundi sanifu

Jeshi la kujenga Taifa(JKT) linawaita vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita mwaka 2024.

Jeshi la kujenga Taifa(JKT) linawaita vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita mwaka 2024.