

Katibu mkuu wizara ya Maji amefungua mkutano wa utambulisho wa mradi mpya unaolenga kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya nchini.
Serikali imezindua mpango wa kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira nchini chini ya mradi wa Shirika lisilo la kiserikali la kimataifa kutoka nchini wingereza SNV kwa kipindi cha miaka minne.
Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika na Katibu mkuu wizara ya Maji Mwajuma waziri jijini Dodoma.
Waziri amesema kuwa Shirika la SNV linafanya kazi katika nchi 20 duniani huku Tanzania ikifanya nao kazi kwa kipindi cha miaka 50 kwenye miradi mitatu tofauti ikiwemo sekta ya Maji,kilimo na nishati ambayo ni uti wa mgongo wa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu na kupunguza umaskini.
"SNV imekuwa ikifanya kazi katika maeneo tofauti ikiwa ni pamoja na mzunguko wa Maji Endelevu ya Mijini unaojumuisha Usafi wa Mazingira na safisha ya Vijijini inayostahimili hali ya hewa, Usimamizi wa Rasilimali za Maji na umwagiliaji Endelevu Jumuishi." Amesema Waziri
Amesema kuwa kati ya mipango ya hivi karibuni ya shirika la SNV katika sekta ya maji ni kuweka mpango wa wash maji ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miaka 6 kwenye mikoa ya Arusha na Shinyanga.
Waziri amesema mpango huo unaenda kusaidia watu zaidi ya laki 2 kwenye kuboresha ya huduma bora za usafi wa mazingira.
Aidha amewataka wadau wengine kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ili kuweza kufanya utekelezaji wa programu hii kuwa na mafanikio makubwa
Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la SNV nchini Tanzania Gloria Kafuria amesema mlengo wao ni kuhakikisha wakala wa maji na mazingira vijini (Ruwasa) wanatoa huduma kitaalam na kuhakikisha mifumo na miondo inatoa huduma kwa wananchi ndani muda.
Vilevile amesema baada ya mradi huo kukamilika kutakuwa na mifumo endelevu japokuwa mifumo ipo ila inahitaji kuboreshwa zaidi ili kuepukana na magonjwa yanayoweza kuepukika.
Kwa upande wa washiriki wakiwakilishwa na Mbogo Fungakamba aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya Maji amesema kuwa serikali inatakiwa itoe elimu kwa wananchi ili kwenda sambamba na mpango huo wa kuinusuru jamii dhidi ya magonjwa yanayo epukika.
WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WAASWA KUZINGATIA MADILI
SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI
WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.
SERIKALI KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA KWA MWAKA WA REJEA 2023.
AZANIA BENKI BUNGE BONANZA LAWALETA PAMOJA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA.
MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUKUTANA KATIKA BONANZA LA KUHAMASISHA MICHEZO NA UMUHIMU WA MAZOEZI.
MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.
RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.
WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.
SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI