DAR ES SALAAM WAELEZA UTAYARI WAO WA KUSHIRIKI KUPIGA KURA, WAYAKATAA MAANDAMANO | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

DAR ES SALAAM WAELEZA UTAYARI WAO WA KUSHIRIKI KUPIGA KURA, WAYAKATAA MAANDAMANO

Wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam wamesema wapo tayari kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, wakijitenga na ushawishi unaofanywa mtandaoni wa kuwataka kuandamana na kutojitokeza kupiga kura, wakieleza kufahamu vyema umuhimu wa amani na athari za vurugu na maandamano ikiwemo vifo, majeraha na kuporomoka kwa uchumi kutokana na kukosekana utulivu wa wao kuendelea na shughuli zao za kiuchumi

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
05 Oct 2025
DAR ES SALAAM WAELEZA UTAYARI WAO WA KUSHIRIKI KUPIGA KURA, WAYAKATAA MAANDAMANO

Wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam wamesema wapo tayari kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, wakijitenga na ushawishi unaofanywa mtandaoni wa kuwataka kuandamana na kutojitokeza kupiga kura, wakieleza kufahamu vyema umuhimu wa amani na athari za vurugu na maandamano ikiwemo vifo, majeraha na kuporomoka kwa uchumi kutokana na kukosekana utulivu wa wao kuendelea na shughuli zao za kiuchumi.

Pantaleo Mushi Mkazi wa Mbezi Beach amesema anafahamu jukumu lake la Kikatiba la kupiga kura, akihamasisha Vijana wengine kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya Kikatiba kupiga kura na kuchagua Kiongozi wamtakaye, akieleza kuwa athari za kutopiga kura ni kuruhusu kuchaguliwa kwa Kiongozi asiyemtaka na kumnyima fursa Kiongozi sahihi kuweza kushika Madaraka kwa kipindi cha miaka mitano ijayo katika Ngazi ya Kata, Jimbo na kwenye Nafasi ya Urais.

Kwa upande wao Said Nassor na Yusuph Ibengwe, wakazi wa Kawe, wameeleza kutofahamu lolote kuhusu maandamano na kusisitiza wananchi kutokubali kurubuniwa katika kuharibu amani ya Tanzania kwa maslahi binafsi ya baadhi ya wanasiasa, wakihimiza wananchi kutumia haki yao vyema ya Kikatiba kuchagua Viongozi wanaowataka kwa njia ya amani hapo Oktoba 29. 2025 siku ya Upigaji kura na kutojihusisha na vurugu ama kusalia vituoni kulinda kura.

Kulingana na baadhi ya wachambuzi wa siasa, mabadiliko yanaanzia kwenye sanduku la kura na ikiwa hutopiga kura, mtu mwingine ataamua hatma yako. Kupiga kura sio haki tu bali ni jukumu lako kama raia kwani unapokaa kimya bila kupiga kura unapoteza haki yako na kuwapa wengine fursa ya kuamua kuhusu maisha yako, serikali yako na mustakabali wa nchi yako. Wanahimiza kutokubali kupoteza sauti yako wakiamini kuwa kura yako ina thamani katika kuitengeneza jamii unayoitaka kwasasa na kizazi kijacho.

Mfalme wa Mashairi Awasha Moto wa Uzalendo: “Kura Yako Ni Silaha”

Mfalme wa Mashairi Awasha Moto wa Uzalendo: “Kura Yako Ni Silaha”

MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.

MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.

DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”

DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”

VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA KUWAKATAA WASIOHESHIMU MISINGI NA TUNU ZA NCHI

VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA KUWAKATAA WASIOHESHIMU MISINGI NA TUNU ZA NCHI

VIJANA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WANAOWEZA KUTIMIZA MATARAJIO YAO

VIJANA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WANAOWEZA KUTIMIZA MATARAJIO YAO