JWTZ: Hatutajihusisha na Siasa, Tunatekeleza Majukumu Yetu Kikatiba | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

JWTZ: Hatutajihusisha na Siasa, Tunatekeleza Majukumu Yetu Kikatiba

Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ limesema kuwa limebaini uwepo wa baadhi ya watu wanaotumia mitandao mbalimbali ya Kijamii kuweka maudhui na ujumbe mbalimbali wenye kuchochea kuliingiza Jeshi hilo katika masuala ya siasa.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
04 Oct 2025
JWTZ: Hatutajihusisha na Siasa, Tunatekeleza Majukumu Yetu Kikatiba

Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ limesema kuwa limebaini uwepo wa baadhi ya watu wanaotumia mitandao mbalimbali ya Kijamii kuweka maudhui na ujumbe mbalimbali wenye kuchochea kuliingiza Jeshi hilo katika masuala ya siasa.

Kaimu Mkurugenzi wa Habari na uhusiano kutoka kwenye Jeshi hilo Makao makuu Kanali Bernad Masala Mlunga amewaambia waandishi wa habari Jumamosi Oktoba 04, 2025 kuwa baadhi ya hoja hizo zinazochapishwa mitandaoni zinatolewa na watu walio katika mazingira ya kijeshi, kujinasibisha na Jeshi pamoja na watu walioachishwa Jeshi kwa kuwa na tabia na mwenendo mbaya pamoja na kujihusisha na siasa na harakati mbalimbali.

Taarifa ya Kanali Mlunga imesisitiza kuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ linaendelea kutekeleza majukumu yake Kikatiba kwa uaminifu, utii na uhodari kwa kuzingatia kiapo chao.

"Jeshi la Wananchi wa Tanzania litaendeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba,kwa uaminifu,utii na uhodari,huku likizingatia misingi ya kiapo cha kijeshi"Amesema Kanali Mlunga

JWTZ wametoa taarifa hiyo siku moja mara baada ya mtu mmoja aliyejitambulisha kama Kapteni wa JWTZ John Charles Tesha, akisema yeye ni Mkufunzi wa zana za anga za kivita katika shule ya Anga (SAK) na akieleza kupitia mtandao wa Youtube kuhusu masuala mbalimbali ya siasa za Tanzania na uchaguzi Mkuu ujao, akitoa shutuma mbalimbali pia kwa baadhi ya Viongozi walioko madarakani na wastaafu, familia zao na watu wao wa karibu, tuhuma ambazo hazina uthibitisho.

Mfalme wa Mashairi Awasha Moto wa Uzalendo: “Kura Yako Ni Silaha”

Mfalme wa Mashairi Awasha Moto wa Uzalendo: “Kura Yako Ni Silaha”

MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.

MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.

DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”

DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”

VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA KUWAKATAA WASIOHESHIMU MISINGI NA TUNU ZA NCHI

VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA KUWAKATAA WASIOHESHIMU MISINGI NA TUNU ZA NCHI

VIJANA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WANAOWEZA KUTIMIZA MATARAJIO YAO

VIJANA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WANAOWEZA KUTIMIZA MATARAJIO YAO