VIWANGO VYA UDUMAVU NA UKONDEVU VIMEPUNGUA NCHINI-MAJALIWA | The Dodoma Post
The Dodoma Post Watoto

VIWANGO VYA UDUMAVU NA UKONDEVU VIMEPUNGUA NCHINI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa kiwango cha udumavu miongoni mwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano nchini kimeshuka kutoka asilimia 48 mwaka 1992 hadi asilimia 30 mwaka 2022.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
30 Sep 2025
VIWANGO VYA UDUMAVU NA UKONDEVU VIMEPUNGUA NCHINI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa kiwango cha udumavu miongoni mwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano nchini kimeshuka kutoka asilimia 48 mwaka 1992 hadi asilimia 30 mwaka 2022.

Ameongeza kuwa, kiwango cha ukondefu miongoni mwa watoto walio chini ya miaka mitano kimepungua kutoka asilimia 5 mwaka 1992 hadi asilimia 3.2 mwaka 2022.

Amesema hayo leo Jumanne (Septemba 30, 2025) wakati alipofunga mkutano wa 11 wa wadau wa lishe nchini, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa APC uliopo Bunju Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua kuwa lishe si suala la kiafya pekee, bali ni nguzo ya maendeleo ya rasilimali watu, uchumi na jamii. “Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na chakula cha kutosha, afya njema na lishe bora”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia ameendelea kuwa kinara wa mapambano dhidi ya utapiamlo kwa kuhakikisha masuala ya lishe yanapewa kipaumbele kwa kuimarisha bajeti, kuboresha mifumo ya ufuatiliaji na uhamasishaji wa afua za lishe kuanzia ngazi ya taifa hadi vijijini.

“Jitihada hizi zilimuwezesha kupata tuzo ya Global Goalkeeper kutoka Taasisi ya Gates Foundation, kutokana na mchango wake mkubwa katika kusukuma mbele Malengo ya Maendeleo Endelevu, hususan kwenye afya ya mama, mtoto na lishe”.

Katika hatua nyingine, mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kiwango cha uzito uliozidi na uzito kupita kiasi (kiribatumbo) hasa miongoni mwa wanawake wa umri wa kuzaa kimeongezeka kutoka asilimia 28 mwaka 2015 hadi asilimia 37 mwaka 2022. “Changamoto hii inaakisi mabadiliko ya ulaji na mtindo wa maisha ulioikumba sio tu Tanzania bali dunia nzima“.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa Wizara na Taasisi zote za umma na binafsi kutenge rasilimali za kutosha kwa ajili ya afua za lishe na kuziweka katika mipango yao ya kila mwaka ili kuongeza uwajibikaji na uendelevu katika kutekeleza mipango iliyopangwa.

Pia Mheshimiwa Majaliwa amezitaka Taasisi za Utafiti na Vyuo vya Elimu ya juu kuendeleza tafiti katika masuala ya lishe pamoja na kuhakikisha ripoti za tafiti hizo zinatumika kuboresha sera na mikakati nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu)Ridhiwan Kikwete amesema kuwa Serikali itahakikisha kuwa wadau wote walioanishwa katika Mpango Jumuishi wa masuala ya Lishe wanaendela kutekeleza majukumu yao. "Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa Wizara zote zinaingiza masuala ya lishe katika mipango ya kibajeti kila mwaka"

Ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imefanikiwa kukamilisha zoezi la utafiti wa gharama za utapiamlo ambao ulilenga kubainisha gharama na athari za utapiamlo katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi

"Matokeo ya utafiti huo yatatumika kama nyenzo muhimu ya uhamasishaji wa viongozi wa juu wa Serikali na watunga sera, kupitia majukwaa mbalimbali ili kuchangia hatua zaidi katika mapambano ya kutokomeza utapiamlo hasa kwa watoto"

Serikali Inaendelea Kuimarisha Mazingira Kuwawezesha Vijana Kuanzisha Shughuli Za Uzalishaji Mali.

Serikali Inaendelea Kuimarisha Mazingira Kuwawezesha Vijana Kuanzisha Shughuli Za Uzalishaji Mali.

FEDHA ZA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU ZIMEONGEZEKA

FEDHA ZA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU ZIMEONGEZEKA

KIDATO CHA NNE 2024 WAITWA KUBADILI MACHAGUO YA TAHASUSI

KIDATO CHA NNE 2024 WAITWA KUBADILI MACHAGUO YA TAHASUSI

MINARA 304 IMEONGEZWA NGUVU KUTOKA 2G KWENDA 3G/4G

MINARA 304 IMEONGEZWA NGUVU KUTOKA 2G KWENDA 3G/4G

JESHI la polisi linawashikilia watu 121 huku 1 kati yao akitekeleza mauaji ya mtoto wa kiume.

JESHI la polisi linawashikilia watu 121 huku 1 kati yao akitekeleza mauaji ya mtoto wa kiume.