

Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila nyumba, jengo, kiwanja, huduma, ofisi ama eneo la biashara linatambulika kwa Anwani ya Makazi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa mawasiliano na teknolojia ya habari Mhe.Jerry Silaa wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya wiki ya anwani za makazi yaliyofanyika ukumbi wa jakaya kikwete jijini Dodoma.
Aidha amesema kuwa Anwani ya Makazi inaundwa na Namba ya Anwani maarufu kama namba ya nyumba; Jina la Barabara au Mtaa; na Postikodi. Postikodi ama nchi zingine zinaita Zipcode ni utaalamu wa kugawa maeneo ili kurahisisha utambuzi. Kwa hapa Tanzania mgawanyo huu umefanyika katika ngazi ya kata ambapo kila Kata ina Postikodi yake yenye tarakimu tano.
Aidha amesema Anwani za Makazi inarahisisha utoaji na upokeaji wa huduma mbalimbali ili kuchochea maendeleo ya Kiuchumi na kijamii hasa katika zama hizi ambazo Mapinduzi ya 4,5 na 6 ya viwanda yanategemea matumizi ya TEHAMA,na matumizi ya TEHAMA yanalazimu kuwa na mifumo ya utambuzi ndiyo sababu ya Serikali kuanzia mfumo huu.
" Itakumbukwa kwamba utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi ulianza mwaka 2010 na kwa mujibu wa Mpango wa utekelezaji ulitakiwa ukamilike mwaka 2015 hata hivyo, utekelezaji wake ulikuwa wa kasi ndogo ukilinganisha na matarijio, hali iliyosababisha kuanzishwa kwa Operesheni maalumu iliyojulikana kama Operesheni Anwani za Makazi ambayo ilizinduliwa na Mheshimiwa Rais, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 08 Februari, 2022"
"Operesheni hiyo ilifanyika nchi nzima na kusimamiwa na wakuu wa mikoa Tanzania Bara na Zanzibar"Ameongeza
Aidha ameongeza kuwa Kufuatia utekelezaji wa Operesheni hiyo, Mfumo wa Anwani za Makazi umeanza kutumiwa na baadhi ya wananchi na taasisi katika kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku; na matunda ama manufaa ya Mfumo yameanza kuonekana ambapo huduma mbalimbali zinatolewa kupitia mfumo wa Anwani za Makazi kama vile barua ya utambulisho ya kidijitali; “Navigation Services”,kuonyesha mahali “locations” . Aidha, elimu inaendelea kutolewa kuhamasisha matumizi hayo.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na Serikali za mitaa(TAMISEMI) Dkt.Festo Dugange akizungumza Kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana Mhe.Mohamed Ncheregwa amesema kuwa Mfumo wa Anwani za Makazi ni nyenzo ya utambuzi ambayo inatambulisha wakazi na makazi na uwepo wa mfumo huu kwa upande wa OR-TAMISEMI ni nyenzo muhimu zaidi kwani kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Serikali za Mitaa, jukumu la kutoa majina ya mitaa lipo OR-TAMISEMI, hivyo utekelezaji wa mfumo huu unarahisisha utekelezaji wa jukumu la kutoa majina ya mitaa kama ambavyo kauli mbiu ya maadhimisho haya inavyosema “TAMBUA NA TUMIA ANWANI ZA KAZI KURAHISISHA UTOAJI NA UPOKEAJI WA HUDUMA”.
Aidha amesema Ofisi ya Rais – TAMISEMI ni mdau mkuu katika utekelezaji hususan kupitia kwa Watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa ambao wana wajibu wa kuwezesha uwekaji wa miundombinu; kuhuisha taarifa; na kukusanya taarifa mpya. Lakini pia TAMISEMI ni mnufaika mkubwa katika matumizi ya Mfumo; hii ni kwa kuzingatia kwamba Mfumo unawezesha utambuzi hivyo hurahisisha utoaji na upokeaji wa huduma.
"TAMISEMI ndiyo yenye wananchi na ndiyo mtoa huduma mkuu kwa wananchi, hivyo TAMISEMI inauhitaji sana Mfumo huu na kwa sasa tulifanya majaribio ya kutoa barua kwa njia ya kidijitali ambapo jambo hilo limeonyesha kuwa la mafanikio"
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.
UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.
MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.
UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.
MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.
GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.
WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.