WIZARA YA NISHATI IPO KWENYE MCHAKATO WA KUZALISHA MBOLEA KWA KUTUMIA GESI ASILIA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Nishati

WIZARA YA NISHATI IPO KWENYE MCHAKATO WA KUZALISHA MBOLEA KWA KUTUMIA GESI ASILIA.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati , Felchesmi Mramba amesema,Wizara ya Nishati ipo kwenye mchakato wa kuzalisha mbolea kwa kutumia gesi asilia ilikuwasaidia wakulima kupata mbolea kwa urahisi na kupunguza gharama ya kuagiza mbolea nje ya nchi.

Moreen Rojas, Dodoma.
By Moreen Rojas, Dodoma.
06 Aug 2024
WIZARA YA NISHATI IPO KWENYE MCHAKATO WA KUZALISHA MBOLEA KWA KUTUMIA GESI ASILIA.

Katibu mkuu Mramba ameeleza hayo alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya petrol(TPDC ) katika viwanja vya maonesho 88 jijini Dodoma ikiwa ni mdau mkubwa wa sekta ya kilimo na Mifugo.

"Kiukweli tumesikia kilio cha wakulima wetu hivyo kama wizara tuko kwenye mchakato wa kuzalisha mbolea kwa kutumia gesi asilia ili kuepuka kuagiza mbolea kutoka nje na kuwapa urahisi wakulima wetu"

Amesema wizara ya Nishati inamchango mkubwa katika kuboresha sekta ya kilimo na sekta  ya ufugaji hasa kwa kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali ambayo shughuli za kilimo na mifugo zinafanyika ikiwemo maeneo ya umwagiliaji.

Katika Banda la wizara ya nishati wananchi wameonesha kuvutiwa na teknolojia ya uhalisia Pepe(virtual reality)ambayo inawezesha wananchi kuona moja kwa moja miradi ya uzalishaji,uchakataji na usambazaji wa gesi asilia iliyopo mkoani mtwara na lindi.

Ameeleza kuwa,  Serikali ya  Tanzania kupitia Sera mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa inatambua umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kama nyenzo muhimu ya kukabiliana na athari za kimazingira, kiafya, kijamii na kiuchumi.

Ameongeza kuwa jitihada hizo za kuelekea kwenye matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia zinafanyika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi.

Kuhusu Maonesho ya Wakulima ya Nanenane, amesema kuwa, yamekuwa ni sehemu ya wananchi kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Sekta ya Nishati ikiwemo miradi ya Gesi Asilia na Mafuta.

Katika hatua nyingine, amesema Sekta ya Nishati inafungamanisha Sekta nyinginezo ikiwemo Madini, Maji, Kilimo na Mifugo ambapo katika Mifugo vinyesi vya wanyama hutumika kuzalisha nishati kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati,  Dkt. James Mataragio ameipongeza Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa kuendelea kutoa elimu ya kwa wananchi kuhusu mafanikio ya Sekta ya  Nishati pamoja na Nishati safi ya kupikia.

Kuhusu Nishati safi ya kupikia tayari elimu imetolewa katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na sekta na wizara mbalimbali na wananchi wamepokea kwa mwitikio mkubwa.

Kiukweli nawashauri wananchi wenzangu waje wajionee mambo mazuri yanayopatikana hapa 88 kwenye mabanda mabalimbali haswa banda la nishati kuweza kujifunza mambo yanayohusiana na nishati safi,binafsi nimejifunza umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia kwajili ya kuhakikisha tunatunza mazingira yetu hivyo niwasihi kina mama wenzangu waje wajifunze"Amesema Habiba Ally mkazi wa Dodoma mjini

BRIGEDIA Jenerali Ngata Apongezwa uongozi makini SUMAJKT

BRIGEDIA Jenerali Ngata Apongezwa uongozi makini SUMAJKT

REA YASAINI MIKATABA YA KUPELEKA UMEME KWENYE VITONGOJI 3,060 KOTE NCHINI

REA YASAINI MIKATABA YA KUPELEKA UMEME KWENYE VITONGOJI 3,060 KOTE NCHINI

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAAHIDI KUUPA MSUKUMO MRADI WA EACOP

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAAHIDI KUUPA MSUKUMO MRADI WA EACOP