KAMPUNI YA ORYX ENERGIES YAZINDUA MFUMO WA USAMBAZI GESI YA LPG KATIKA SOKO LA SAMAKI FERI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

KAMPUNI YA ORYX ENERGIES YAZINDUA MFUMO WA USAMBAZI GESI YA LPG KATIKA SOKO LA SAMAKI FERI.

KAMPUNI ya ORYX Energies Tanzania imezindua mfumo wa kwanza wa usambazaji wa gesi ya LPG kwa wingi katika Soko la Samaki la Kimataita Ferry jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
21 Aug 2025
KAMPUNI YA ORYX ENERGIES YAZINDUA MFUMO WA USAMBAZI GESI YA LPG KATIKA SOKO LA SAMAKI FERI.

KAMPUNI ya ORYX Energies Tanzania imezindua mfumo wa kwanza wa usambazaji wa gesi ya LPG kwa wingi katika Soko la Samaki la Kimataita Ferry jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mradi huo wa kihistoria umezinduliwa leo.Agosti 21,2025 jijini Dar se salaam ambapo hiyo ni hatua kubwa katika kuimarisha upatikanaji wa nishati safi kwa wauzaji wa samaki na wajasiriamali wadogo katika soko hilo ambapo sasa mfumo huo unaweza kulipia kadri ya matumizi (PAYG), unaowawezesha wauzaji kulipia gesi wanayotumia tu na hivyo kuondoa gharama kubwa za kujaza mitungi na kupunguza matumizi ya kila siku hadi Sh.45,000.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo huo ambapo limejengwa tanki kubwa ambalo linatumika kusambaza gesi katika majiko ya wafanyabiashara hao,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema mfumo huo sasa utawezesha kulipa kulingana na matumizi yako.

Amesema kila mfanyabiashara sasa ana mita yake inayosoma matumizi yake ya kila siku, kabla na baada ya matumizi. Hakuna tena kubahatisha, hakuna tena kulazimika kununua mitungi midogo kwa gharama kubwa.

Pia amesema Oryx wamezingatia usalama,kwa kufunga valve ambazo itatumika kufunga gesi endapo itatokea dharulakwa kila jiko. Tunafahamu matumizi makubwa hivi ya gesi yanahitaji  usalama wa hali ya juu.

Pia amesema viwango vya matumizi gesi vitafuatiliwa kwa urahisi ili kuhakikisha gesi inaletwa kujaza kwenye hili tanki kubwakwa wakati huku akieleza gharama imepungua na wafanyabiashara waliokuwa wakitumia hadi Sh.180,000 kujaza gesi kwa siku sasa wanaweza kuokoa hadi Sh.45,000 kila siku. 

“Kupitia mfumo wa Lipa Kadri Unavyotumia,hili ni suala la kupongezwa sana.Hakuna upotevu, hakuna gesi isiyotumika tofauti na zamani ambapo mtungi mdogo mliotumia wakati fulani gesi inabaki kidogo. Usalama wa Juu, hili sina shaka na utalamu wenu Oryx kwenye suala zima la usalama.Nafahamu tahadhari zote zimezingatiwa hasa kwa kuweka Vifaa vya kuzima moto nataratibu za dharura zipo tayari.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Benoit Araman amesema lengo la kuwa na mfumo huo wa kuwa na tanki la gesi katika soko hilo unalenga kupunguza  gharama za kujaza, kupunguza upotevu, na kuongeza ufanisi

Usalama  Mfumo usiovuja

Amesema ni mfumo wa kisasa uliofanywa na team ya ufundi ya Oryx gas kwa kuzingatia kanuni za kitaifa na kimataifa.Pia urahisishaji wa Uendeshaji Ugavi endelevu pamoja na ufuatiliaji wa kisasa, na matengenezo madogo.

Awali Kamishina wa Nishati Mhandisi Innocent Luoga kutoka Wizara ya Nishati ameeleza hatua mbalimbali ambazo zinaendelea kuchukuliwa na Serikali katika kufanikisha mpango wa nishati safi huku akiiipongeza Oryx kwa hatua inazoendelea kuchukua katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

“Tangu mkakati wa kitaifa ulipozinduliwa Januari mwaka 2024  wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kumekuwepo na mafanikio makubwa na ongezeko la matuminizi ya majiko ya gesi yamekuwa makubwa,”amesema Mhandisi Luoga na kufafanua mkakati wa Serikali ifikapo mwaka 2034 asilimia  80 ya wananchi wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

Katika hatua nyingine aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Ilala Dar es Salaam Mussa Zungu amesema awali wafanyabiashara wa soko hilo walimfikishia mahitaji yao hivyo aliwatafuta Oryx Gas na leo amefurahi kuona umefungwa mfumo huo ambao unakwenda kurahisisha shughuli za wafanyabiashara hao.

Zungu amesema tafiti zinaonesha duniani  kuwa Kuna vifo vingi vinavyotona na Matumizi ya Nishati isio salama hivyo Mradi huu unakwenda kuwa majawabu ya kuimarisha Afya za wadau hao."Lengo nikufanya biashara kwa amani katika eneo hili lakini ametaka kuendelea kutoa elimu juu ya Mradi huo."

MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA

MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA

SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MGODI NYANDOLWA.

SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MGODI NYANDOLWA.

SERIKALI YAENDELEA NA JITIHADA ZA UOKOAJI MGODI WA NYANDOLWA

SERIKALI YAENDELEA NA JITIHADA ZA UOKOAJI MGODI WA NYANDOLWA

MHANDISI SANGA AONGEZA MWEZI MMOJA KLINIKI YA ARDHI KIVULE KUONGEZA KASI YA UTOAJI HATI

MHANDISI SANGA AONGEZA MWEZI MMOJA KLINIKI YA ARDHI KIVULE KUONGEZA KASI YA UTOAJI HATI

Kwa Miaka 4 MSD Imefikisha Vituo 8776 Ikiwa Ni Ongezeko La Vituo 1681.

Kwa Miaka 4 MSD Imefikisha Vituo 8776 Ikiwa Ni Ongezeko La Vituo 1681.