SERIKALI Imeendelea Kujenga na Kuboresha Miundombinu ya Viwanja vya Ndege | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

SERIKALI Imeendelea Kujenga na Kuboresha Miundombinu ya Viwanja vya Ndege

Serikali imeendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege nchini ambapo Viwanja vya ndege vilivyokamilika ni,ujenzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Songwe, Mtwara, Songea, Iringa Awamu ya I na kiwanja cha ndege cha Geita.

Moreen Rojas (Dodoma)
By Moreen Rojas (Dodoma)
06 May 2025
SERIKALI Imeendelea Kujenga na Kuboresha Miundombinu ya Viwanja vya Ndege

Waziri wa Ujenzi Mhe.Abdallah Ulega ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma tarehe 5 Mei 2025 wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya ujenzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Aidha utekelezaji wa miradi mingine ya viwanja vya ndege ni Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Package I (asilimia 87) na 
Package II (asilimia 53.2); Kiwanja cha Ndege cha Kigoma (asilimia 20); Kiwanja cha Ndege cha Tabora (asilimia 93), Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga (asilimia 60), Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga (asilimia 80) na Kiwanja cha Ndege cha Musoma (asilimia 58).

Aidha katika mwaka wa fedha 2024/25, Wizara ya Ujenzi ilitengewa Shilingi 81,407,438,000.00 ikiwa ni Bajeti ya Matumizi ya 
Kawaida,kati ya fedha hizo, Shilingi 76,588,233,000.00 ilikuwa ni Bajeti ya Mishahara na Shilingi 4,819,205,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo.

Hadi Aprili, 2025 jumla ya Shilingi 63,506,309,562.24 zilipokelewa,Kati ya fedha hizo, Shilingi 61,152,975,329.92 ni kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi wa Wizara na Taasisi na Shilingi 2,353,334,232.32 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo ya Wizara na Taasisi zake.

Bajeti kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo iliyotengwa kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa Wizara ya Ujenzi ni Shilingi 1,687,888,714,000.00. Kati ya fedha hizo, Shilingi 1,141,803,989,000.00  ni fedha za ndani na Shilingi 546,084,725,000.00 ni fedha za nje.

"Kati ya fedha za ndani, Shilingi 599,756,467,800.00 ni fedha zilizotengwa kwa ajili ya bajeti ya Mfuko wa Barabara na Shilingi 
542,047,521,200.00 ni fedha kutoka katika Mfuko Mkuu wa Serikali"

"Hadi Aprili, 2025 fedha zilizopokelewa ni Shilingi 1,535,092,021,470.55. Kati ya fedha hizi, Shilingi   944,881,583,335.76 ni fedha za ndani na Shilingi 590,210,438,134.79 ni fedha za nje,kati ya fedha za ndani zilizopokelewa, Shilingi 482,085,328,011.98 ni kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali na Shilingi 462,796,255,323.78 ni za Mfuko wa Barabara"

Aidha Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS inasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 37,435.04.  Kati ya hizo kilometa 
12,527.44 ni barabara kuu na kilometa 24,907.60 ni barabara za mikoa.

Katika mwaka wa fedha 2024/25, miradi ya barabara kuu iliyopangwa kutekelezwa ni ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara zenye urefu 
wa kilometa 385, ukarabati wa kilometa 35 kwa kiwango cha lami, ujenzi wa madaraja 17, ukarabati wa daraja moja (1), maandalizi ya ujenzi wa madaraja tisa (9) na Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa madaraja mawili (2).

Hadi kufikia Aprili, 2025, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara zenye urefu wa kilometa 109.49 umekamilika na ujenzi wa kilometa 
275.51 unaendelea.

Kwa upande wa madaraja, ujenzi wa madaraja  matano (5) unaendelea na ujenzi wa madaraja  matano (5) upo katika hatua za maandalizi,Vilevile, taratibu za ununuzi ya Makandarasi wa ujenzi wa madaraja matano (5)zinaendelea,Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa madaraja 11 na ukarabati wa daraja 1 katika mikoa mbalimbali nchini.

Sanjari na hayo hadi Aprili, 2025 jumla ya kilometa 98.13 za barabara za mikoa zilijengwa kwa kiwango cha lami na jumla ya kilometa 192.9 zilikarabatiwa kwa kiwango cha changarawe.

Aidha, ujenzi/ukarabati wa madaraja madogo 7 kwa kutumia fedha za Mfuko Mkuu wa Serikali na 9 kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara umekamilika na madaraja 91 yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Rais Samia Asisitiza Mchujo wa Wagombea Kufanyika Kwa Haki.

Rais Samia Asisitiza Mchujo wa Wagombea Kufanyika Kwa Haki.

WIZARA YA ARDHI YAJA NA VIPAUMBELE SABA

WIZARA YA ARDHI YAJA NA VIPAUMBELE SABA

Wananchi Dodoma Waaswa kuchangamkia Fursa kuelekea Mkutano Mkuu CCM

Wananchi Dodoma Waaswa kuchangamkia Fursa kuelekea Mkutano Mkuu CCM

Wizara Inaendelea Kutekeleza Programu ya BBT Kwa Vijana Kuwawezesha Kujiajiri

Wizara Inaendelea Kutekeleza Programu ya BBT Kwa Vijana Kuwawezesha Kujiajiri

Wizara Imeimarisha Matumizi ya Mfumo wa Portal ya HAKI SHERIA Unaotumiwa na Wananchi Kupata Msaada

Wizara Imeimarisha Matumizi ya Mfumo wa Portal ya HAKI SHERIA Unaotumiwa na Wananchi Kupata Msaada