

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anatoa wito Kwa vijana waliohitimu elimu ya Sekondari Kidato Cha Sita kwa mwaka 2025,kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT Kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2025
Hayo yameelezwa na Kanali Juma Mrai Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT wakati akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 27 Mei 2025 Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dodoma.
Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayo kwenda kupatiwa Mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 28 Mei 2025 hadi tarehe 08 Juni 2025.
Aidha Vijana hao wamepangwa katika Kambi za JKT zifuatazo; JKT Rwamkoma - Mara,JKT Msenge- Tabora,JKT Ruvu na JKT Kibiti - Pwani,JKT Mpwapwa, JKT Makutupora - Dodoma,JKT Mafinga - Iringa,JKT Male - Ruvuma,JKT Mgambo na JKT Maramba - Tanga,JKT Makuyuni na JKT Orjolo - Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila - Kigoma,JKT Itaka - Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa - Rukwa pamoja na JKT Nachingwea - Lindi.
"Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana Kwa macho(Physical Disabilities) waripoti katika Kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo"
Aidha JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na Bukta ya Dark Bluu yenye mpira kiunoni(lastic)iliyo na mfuko mmoja nyuma,urefu unaoishia magotini,isiyo na zipu, T-shirt rangi ya kijani,Raba za Michezo zenye rangi ya kijani na Bluu,shuka mbili za kulalia zenye rangi ya Bluu bahari,soksi ndefu za rangi nyeusi,Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi,Track suit ya rangi ya kijani au Bluu,Nyaraka zote zinazohitajika katika udahili wa kujiunga na elimu ya juu,zikiwemo Cheti Cha kuzaliwa,vyeti vya kuhitimu kidato Cha Nne,nauli ya kwenda kuripoti makambini na kurudi nyumbani.
"Orodha kamili ya majina ya vijana hao,Makambi ya JKT waliopangiwa na maeneo makambi hayo yalipo na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo,inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.mil.tz"
Aidha ili kufahamu Kambi kijana aliyopangiwa,atatakiwa kuingiza jina la Shule au namba ya Shule aliyohitimu elimu ya kidato Cha Sita,mbele ya jina lake la Shule ataona neno lililoandika waliochaguliwa,akichagua neno hilo ataona jina au majina ya waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya JKT Kwa Mujibu wa sheria kwa mwaka 2025,ikionesha kambi aliyopangiwa,Mkoa na wilaya ilipo kambi hiyo.
"Ili kuona majina yote ya vijana na Kambi waliopangiwa,mtumiaji atapakua JKT PDF 2025 iliyopo juu kulia katika ukurasa huo"
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele anawakaribisha Vijana wote waliohitimu kidato Cha Sita mwaka 2025 kuungana na Vijana wenzao ili kujengewa uzalendo,Umoja wa Kitaifa,kufundishwa stadi za kazi,stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa lao.
Rais Samia Asisitiza Mchujo wa Wagombea Kufanyika Kwa Haki.
Ilani Ya CCM Imeandaliwa Kwa Weledi Mkubwa Kwa Kushirikiana Na Wananchi;RAIS Dkt.Samia
WIZARA YA ARDHI YAJA NA VIPAUMBELE SABA
SERIKALI NA WADAU WAENDELEZA MAPAMBANO YA KIJINSIA
KAPINGA ATAJA VIGEZO VYA ZIADA UPELEKAJI UMEME VITONGOJINI.
WIZARA YA ARDHI YAJA NA VIPAUMBELE SABA
Ilani Ya CCM Imeandaliwa Kwa Weledi Mkubwa Kwa Kushirikiana Na Wananchi;RAIS Dkt.Samia
SERIKALI NA WADAU WAENDELEZA MAPAMBANO YA KIJINSIA
Rais Samia Asisitiza Mchujo wa Wagombea Kufanyika Kwa Haki.
Vijana Kutoka Kenya Waonywa Vikali Kuacha Kumkejeli Rais Samia Katika Mitandao ya Kijamii