Wizara Imetekeleza Mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Milki za Ardhi(LTIP) | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

Wizara Imetekeleza Mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Milki za Ardhi(LTIP)

Mradi huu umewezesha uhakiki wa mipaka ya vijiji 871 na uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 846 katika Halmashauri 21.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
23 May 2025
Wizara Imetekeleza Mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Milki za Ardhi(LTIP)

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe.Deogratius Ndejembi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita tarehe 23 Mei 2025 katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma.

Aidha jumla ya vipande vya ardhi 583,734 vimehakikiwa na vimepandishwa katika mfumo wa e-Ardhi, Vilevile, Hati za Hakimiliki za Kimila 318,868 zimesajiliwa katika vijiji 236 vya Wilaya sita (6) za Songwe, Chamwino, Mufindi, Mbinga, Maswa na Tanganyika,Mradi huu pia umewezesha urasimishaji wa makazi 136,129 katika Halmashauri za Jiji la Dodoma; Wilaya za Chalinze na Songea; Manispaa za Kahama, Shinyanga, Kigoma na Mtwara; na Mji wa Nzega.

"Kazi nyingine zilizotekelezwa kupitia Mradi ni uwekaji wa Alama za Msingi za Upimaji 427 katika Halmashauri 35; kuanza ujenzi wa vituo 22 vya kielekroniki vya upimaji ardhi; na uandaaji wa mfumo wa kidijiti wa vitalu vya thamani nchini"

Vilevile, Mradi umewezesha Halmashauri 13 kutumia mfumo wa e-Ardhi, hivyo kuboresha usimamizi wa taarifa za ardhi kwa njia ya kidijiti. Pia, Mradi umewezesha upatikanaji wa vitendea kazi yakiwemo magari 70 kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma za ardhi.

Aidha, Serikali imeiwezesha Wizara kutekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Miundombinu ya Upimaji na Ramani (LDI) wenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 65.

"Mradi huu unalenga kuimarisha miundombinu ya upimaji na ramani kwa kujenga Vituo vya Kielektroniki vya Upimaji 30; kununua ndege maalum ya upigaji wa picha za anga; na ununuzi wa vifaa vya upimaji"

"Utekelezaji wa mradi huu utaongeza kasi ya upangaji na upimaji ardhi sambamba na kuimarisha matumizi ya ramani hizo katika utekelezaji wa miradi ya Serikali. Ramani za msingi zitaandaliwa kwa uwiano wa 1:2,500 katika miji mikuu ya mikoa na uwiano wa 1:25,000 kwa nchi nzima"Amesema

Aidha kwa kuzingatia kwamba sekta ya ardhi ni sekta wezeshi kwa sekta nyingine, Wizara imeendelea kushiriki katika miradi ya kitaifa ya kimkakati kwa kupanga na kupima maeneo inapotekelezwa miradi ya Kitaifa.

Miradi hiyo ni ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP), ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) lenye urefu wa kilometa 1,146 kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanga Tanzania na ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR).  Vilevile, Wizara ilishiriki kwenye matukio mbalimbali ya kitaifa ikiwemo utwaaji, uthamini, upangaji upimaji na umilikishaji wa ardhi kwa ajili ya waathirika wa maporomoko ya mlima Hanang’ mkoani Manyara.

Sanjari na hayo katika kipindi cha awamu ya Sita, Wizara imepokea shilingi bilioni 64.5 kwa ajili ya kutekeleza Programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK) katika Halmashauri 131 ikiwemo shilingi bilioni 50 zilizokopeshwa kwenye Halmashauri 57 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Ardhi (Plot Development Revolving Fund (PDRF)ambapo Fedha hizo zimewezesha upangaji na upimaji wa viwanja 556,191.

SERIKALI NA WADAU WAENDELEZA MAPAMBANO YA KIJINSIA

SERIKALI NA WADAU WAENDELEZA MAPAMBANO YA KIJINSIA

Siku Ya Utumishi wa Umma, Watumishi Kufanya Maonesho ya Kutambua Mchango na Umuhimu wao Kwenye Jamii.

Siku Ya Utumishi wa Umma, Watumishi Kufanya Maonesho ya Kutambua Mchango na Umuhimu wao Kwenye Jamii.

Vijana Kutoka Kenya Waonywa Vikali Kuacha Kumkejeli Rais Samia Katika Mitandao ya Kijamii

Vijana Kutoka Kenya Waonywa Vikali Kuacha Kumkejeli Rais Samia Katika Mitandao ya Kijamii

WIKI YA AZAKI KUADHIMISHWA ARUSHA JUNI 2 HADI 6 WADAU WA MAENDELEO KUSHIRIKI.

WIKI YA AZAKI KUADHIMISHWA ARUSHA JUNI 2 HADI 6 WADAU WA MAENDELEO KUSHIRIKI.