

Wizara imeimarisha matumizi ya mfumo wa Portal ya HAKI SHERIA ambao unatumiwa na wananchi na maafisa Dawati la Msaada wa Kisheria katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 184 nchini
Hayo yameelezwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dkt.Damas Ndumbaro wakati akizungumza na waandishi wa habari Mei 20 katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo kuhusu mafanikio ya Wizara hiyo ndani ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.
Aidha amesema Katika kurahisisha tafsiri ya hukumu na kumbukumbu za mashauri, Mahakama imejenga Mfumo wa Kunukuu na Kutafsiri Kumbukumbu za Kimahakama wenye uwezo wa kutafsiri kumbukumbu za kimahakama kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili.
Aidha Mahakama inafanya utaratibu wa kutumia mfumo wa kutafsiri katika Mahakama zote zenye miundombinu ya internet nchini.
"Ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati na gharama nafuu, Serikali imeendelea kufungua ofisi mpya za Mashtaka katika Wilaya ambapo ofisi hizo zimeongezeka kutoka 53 mwaka 2021 hadi 108 mwaka 2025"
Katika kipindi cha mwaka 2021 hadi mwaka 2025, Serikali imesajili jumla ya watoa huduma 123 walioomba kuthibitishwa kama Watoa Huduma za Utatuzi wa Migogoro kwa njia mbadala, hadi Aprili, 2025 wapo Watatuzi wa Migogoro kwa Njia Mbadala 498, kati ya hao, Watoa Huduma za Majadiliano 222, Wapatanishi 174, Wasuluhishi 37 na Waendesha Maridhiano 65.
Aidha Serikali kupitia Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini umesajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano ambapo hadi kufikia Aprili, 2025 watoto 10,824,267 wamesajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.
"Tanzania inazingatia masuala ya haki za binadamu na utawala bora ikiwa ni pamoja na Serikali kuiwezesha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutekeleza majukumu yake kikamilifu, Machi 2023, Taasisi Inayosimamia Haki za Binadamu Duniani imeipatia Daraja “A” Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora"
Katika kipindi cha mwaka 2021 hadi mwaka 2025, sheria mbalimbili zimetungwa na kufanyiwa marekebisho ikiwemo Sheria Kuu 57 na Sheria Ndogo 4,087.
Katika kipindi cha mwaka 2021 hadi mwaka 2025, Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania ilisajili jumla ya wanafunzi 5,333 sawa na asilimia 28 ya wanafunzi 19,025 waliosajiliwa katika miaka 18 tangu kuanzishwa kwa Taasisi.
Aidha, katika kipindi hicho, Taasisi ilitoa wahitimu 2,375 sawa na asilimia 25 ya wahitimu 9,629 waliohitimu tangu kuanzishwa kwa Taasisi mwaka 2008. Hivyo, jumla ya Mawakili 2,375 wameongezeka katika Sekta ya Sheria.
"Katika kipindi cha mwaka 2021 hadi mwaka 2025, jumla ya wanafunzi 2,876 wamehitimu mafunzo katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama wakiwemo 1,553 katika ngazi ya cheti na 1,323 katika ngazi ya astashahada"
Sanjari na hayo Serikali imeanzisha Kituo cha Huduma kwa Mteja ambapo mwananchi hupata fursa ya kuwasilisha malalamiko na hoja mbalimbali za kisheria moja kwa moja kupitia namba ya simu 0262160360, namba ya Whatsapp 0739101910 na barua pepe kupitia malalamiko@sheria.go.tz.
Aidha Katika kipindi cha 2021 hadi 2025, idadi ya Majaji imeongezeka kutoka 92 (Mahakama Kuu – 76 na Mahakama ya Rufani - 16) kufikia 146 (Mahakama Kuu – 107 na Mahakama ya Rufani - 39). Pia, idadi ya Mahakimu imeongezeka kutoka 1,412 Aprili, 2021 kufikia Mahakimu 1,426 Aprili, 2025.
"Mashauri yenye umri mrefu Mahakamani ni 2,780 sawa na asilimia 4 ya mashauri yote yaliyobaki Mahakamani. Hivyo, Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye mrundikano mdogo wa mashauri Mahakamani"
"Ujenzi wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki sita umekamilika katika maeneo ya Dodoma, Morogoro, Mwanza, arusha, Kinondoni na Temeke. Aidha, ujenzi wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki tisa (9) unaendelea katika mikoa mbalimbali"
Aidha Ujenzi wa majengo ya Mahakama za Wilaya tatu umekamilika. Aidha, ujenzi wa majengo ya Mahakama za Wilaya 11 unaendelea.
"Ujenzi wa Mahakama za Mwanzo 26 umekamilika na ujenzi wa Mahakama za Mwanzo 72 unaendelea. Ukarabati wa jengo la zamani la Mahakama Kuu Dodoma umefikia asilimia 57. Aidha, ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama lililopo Dodoma umekamilika na kuzinduliwa tarehe 05 Aprili, 2025"
Aidha Ujenzi wa nyumba za Majaji eneo la Iyumbu, Dodoma umekamilika na kuzinduliwa tarehe 05 Aprili, 2025. Ujenzi wa nyumba ya Jaji Mkuu, jijini Dodoma unaendelea ambapo ujenzi umefikia asilimia 56.
Serikali imeendelea kuboresha mifumo ya TEHAMA katika utoaji huduma za kisheria ambapo hadi kufikia Aprili, 2025; asilimia 75 ya mifumo ya TEHAMA katika Sekta ya Sheria imeunganishwa.
Rais Samia Asisitiza Mchujo wa Wagombea Kufanyika Kwa Haki.
Ilani Ya CCM Imeandaliwa Kwa Weledi Mkubwa Kwa Kushirikiana Na Wananchi;RAIS Dkt.Samia
WIZARA YA ARDHI YAJA NA VIPAUMBELE SABA
SERIKALI NA WADAU WAENDELEZA MAPAMBANO YA KIJINSIA
KAPINGA ATAJA VIGEZO VYA ZIADA UPELEKAJI UMEME VITONGOJINI.
WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WAITWA JKT
WIZARA YA ARDHI YAJA NA VIPAUMBELE SABA
Ilani Ya CCM Imeandaliwa Kwa Weledi Mkubwa Kwa Kushirikiana Na Wananchi;RAIS Dkt.Samia
SERIKALI NA WADAU WAENDELEZA MAPAMBANO YA KIJINSIA
Rais Samia Asisitiza Mchujo wa Wagombea Kufanyika Kwa Haki.