GAVANA TUTUBA: RIBA YA BENKI KUU KUENDELEA KUWA ASILIMIA 6. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

GAVANA TUTUBA: RIBA YA BENKI KUU KUENDELEA KUWA ASILIMIA 6.

Kamati ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuendelea na kiwango cha Riba ya Benki Kuu (CBR) cha asilimia 6 kwa robo ya kwanza ya mwaka 2025.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
08 Jan 2025
GAVANA TUTUBA: RIBA YA BENKI KUU KUENDELEA KUWA ASILIMIA 6.

Kamati ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuendelea na kiwango cha Riba ya Benki Kuu (CBR) cha asilimia 6 kwa robo ya kwanza ya mwaka 2025.

“Uamuzi huo wa Kamati wa kutokubadili Riba ya Benki Kuu unalenga kuhakikisha kiwango cha ukwasi kinaendelea kuwa cha kutosha katika uchumi, kudhibiti mfumuko wa bei kubaki chini ya lengo la asilimia 5, na kuwezesha kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi kufikia takriban asilimia 5.7 katika robo ya kwanza ya mwaka 2025,” amesema Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba.

Alikuwa akitangaza uamuzi huo mbele ya wakuu wa benki na taasisi za fedha pamoja na waandishi wa habari tarehe 8 Januari 2025 jijini Dar es Salaam kufuatia kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha kilichofanyika tarehe 7 Januari.

Aidha, uamuzi huo ambao umefikiwa kutokana na tathmini iliyofanywa ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini, unalenga kuwa na utulivu wa thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni ili kuendelea kuwa na mfumuko wa bei mdogo.

“Utulivu wa thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni utachangia katika juhudi za kufanya wananchi kutofanya miamala kwa kutumia fedha za kigeni nchini,” amese Gavana Tutuba.

Kuhusu mwenendo wa uchumi wa dunia, Kamati ya Sera ya Fedha imesema ripoti za Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia, zinaonesha ukuaji wa uchumi unakadiriwa kuwa imara katika mwaka 2024.

Aidha, mazingira ya uchumi duniani katika robo ya nne ya mwaka 2024 yaliimarika kwa kiwango kikubwa, ambapo kasi ya ukuaji wa uchumi iliongezeka, mfumuko wa bei uliendelea kupungua katika nchi nyingi, na mazingira ya upatikanaji wa fedha kwa riba nafuu katika masoko yaliimarika.

Hata hivyo, matarajio hayo mazuri ya uchumi yanaweza kuathirika endapo migogoro ya kisiasa duniani na mivutano ya kibiashara itaongezeka.

SAYANSI YA BAHARI NGUZO YA UCHUMI WA BLUU-RAIS MWINYI

SAYANSI YA BAHARI NGUZO YA UCHUMI WA BLUU-RAIS MWINYI

Watumishi wa Umma Waaswa kujifunza mifumo mipya ya Tehama ili kuwafikia wananchi kwa ukaribu.

Watumishi wa Umma Waaswa kujifunza mifumo mipya ya Tehama ili kuwafikia wananchi kwa ukaribu.

BoT KUJA NA MFUMO WA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA KIFEDHA KIDIGITAL.

BoT KUJA NA MFUMO WA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA KIFEDHA KIDIGITAL.

UZINDUZI WA TEKNOLOJIA MPYA YA UREKEBISHAJI NA UTUNZAJI WA MAGARI  KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI.

UZINDUZI WA TEKNOLOJIA MPYA YA UREKEBISHAJI NA UTUNZAJI WA MAGARI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI.

THE WHEEL YALETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI NCHINI.

THE WHEEL YALETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI NCHINI.