Jamii yaaaswa kutumia nishati safi ili kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha kila mtanzania anatumia nishati safi ili kulinda mazingira na kuendana na kasi ya kukua kiuchumi na teknolojia.
Hayo yameelezwa na Dkt.Kenneth Nzowa ambaye ni Mkuza Mitaala Mwandamizi kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania Dar es Salaam katika Kongamano la 16 la wanazuoni lililofanyika katika Chuo Cha Serikali za Mitaa kampasi kuu Hombolo jijini Dodoma huku mada kuu ikiwa "Nishati safi,changamoto zilizopo na uwezekano wa kuhamasisha wananchi kufanya kama sehemu ya maendeleo yao"
Aidha amesema kuwa wanatoa elimu Kwa watu mbalimbali na wanaamini mtu anapopata elimu atakuwa anajua kwamba kutumia nishati kwa ajili ya maendeleo binafsi mfano mabomba ya umwagiliaji yanayotumia umeme,majiko ya gesi ambayo ndio nishati safi ya kupikia kwani vijijini watu wengi bado hawaelewi kuhusu matumizi ya nishati safi na faida yake ikiwemo rafiki wa mazingira.
Aidha ameongeza kuwa wanapoongelea kuhusu nishati safi hawaongelei umeme tu pia wanazungumzia namna ya kuhakikisha kina mama wanapika kisasa Kwa kuweza kuwahamasisha mama lishe kutoka kwenye kutumia Kuni na mkaa hadi nishati safi na mfano mzuri amekuwa akiuonesha Rais kwa kusambaza gesi kwa kina Mama.
"Ni kweli gharama za Sola zinafanya watu wengi waogope kutumia lakini suala zuri ni kwamba ukilipia mara moja na ukizingatia wananchi wengi wana saccos ambazo zinawasaidia kupata pesa na ikiwa ni njia nzuri kwa kila mmoja kupata nishati safi"Amesisitiza
Aidha ameishauri Serikali kuangalia namna bora ya kupunguza kodi kwenye viwanda vya Sola ili kuhakikisha kila mwananchi anaendana na kasi ya ukuaji kiuchumi Kwa kutumia nishati safi.
Kwa Upande wake Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma,Tafiti na Ushauri Professa Magreth Bushesha amesema mkutano huo ni wanazuoni waliosoma Chuo Cha Hombolo na wanaoendelea kusoma ambapo kazi ya wanazuoni ni kuchakata mada mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Aidha amesema Nishati safi inahamasishwa Kwa ajili ya kwenda na ulimwengu wa kisasa na rafiki mzuri wa mazingira hivyo wakaona ni muhimu kulileta Kwa wanazuoni Kwa kuweza kuhakikisha ni namna gani wanawasaidia watanzania juu ya matumizi safi ya nishati.
"Jukumu kubwa la wasomi wa nchi hii ni kuweza kuhakikisha wanawasaidia watanzania kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kama taifa ili kufika muafaka na kuona ni namna gani tunaweza kuwahamasisha watanzania umuhimu wa nishati safi ili tuweze kuwa rafiki wa mazingira na kuendana na kasi ya ulimwengu tuliopo"Ameongeza
Naye Nicholaus Rugarabamu Mwanafunzi wa Shahada ya Usimamizi wa Rasilimali watu mwaka wa kwanza kutoka katika Chuo hicho aliyepata tuzo ya Mwanafunzi Bora amesema anajiskia furaha kupata tuzo hiyo ambayo imetokana na juhudi zake binafsi kusoma Kwa bidii na kumtanguliza Mungu bila kusahau kushirikiana na wanafunzi wenzake.
"Siri ya mafanikio ya tuzo ni kujituma kusikiliza walimu na uwezo binafsi na Mungu ndo kila kitu lakini Kwa ambao hamjapata msijiskie vibaya naomba tuzo hii iwe chachu kwenu kusoma kwa bidii ili nanyi muweze kupata tuzo hii"Amesema Salma Hamisi Mwanafunzi wa Shahada ya Usimamizi wa Rasilimali watu mwaka wa pili.
MENEJIMENTI YA MOI YAWAPA ZAWADI NA SHUKURANI WATUMISHI WAKE
Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.
Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.
HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO
DAR CITY YAING’ARISHA TANZANIA MASHINDANO YA KIKAPU AFRIKA MASHARIKI