Wachimbaji wa Madini wahimizwa kulipa kodi ya Serikali. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

Wachimbaji wa Madini wahimizwa kulipa kodi ya Serikali.

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ametatua mgogoro wa wachimbaji wadogo wa Madini ya Ruby Wilaya ya Longido Mkoani Arusha uliodumu kwa zaidi ya miaka mitano kati ya Kampuni ya Paradiso Mineral (T) Limited na Mzee Malulu Ole.

The Dododma Post
By The Dododma Post
07 Dec 2024
Wachimbaji wa Madini wahimizwa kulipa kodi ya Serikali.

Makubaliano hayo yameafikiwa jana Desemba 6, 2025 wakati Dkt. Kiruswa alipofanya ziara ya kutatua mgogoro huo katika Kata ya Mundarara Wilaya ya Longido Mkoani Arusha. 

Mhe. Dkt. Kiruswa ameielekeza kampuni ya Paradiso kutekeleza makubaliano walioafikiana na Mzee Malulu Ole Moringo ya kulipa fidia hiyo kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza wanatakiwa kulipa milioni 100 ifikapo Januari 30, 2025 na milioni 50 ifikapo Machi 30, 2025.

Aidha, Dkt. Kiruswa amesisitiza makubaliano hayo kutekelezwa kwa wakati na endapo kampuni ya Paradiso itakiuka makubaliano hayo Serikali itachukua hatua za kisheria ikiwemo kusimamisha shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.

Sambamba na hayo, Dkt. Kiruswa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na  Dkt. Samia Suluhu Hassan haitaki migogoro katika sekta ya Madini ili sekta hiyo kuwa na  maendeleo.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Kiruswa amewataka wachimbaji wa madini kuendelea kulipa kodi za Serikali ambapo fedha hizo zitakwenda kuboresha huduma za kijamii kama vile kujenga shule na usambazaji wa umeme maeneo mbalimbali hapa nchini.Awali, Ofisi ya Madini Arusha ilifanya utafiti na kugundua Malulu Ole Moringo ana haki katika eneo hilo ambalo familia ya Jango Master inafanya shughuli za uchimbaji Madini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha (CCM) Papaanakuta Moleli amempongeza Dkt. Kiruswa kwa kazi nzuri anazozifanya za kutatua migogoro mbalimbali ya wachimbaji wa Madini  hapa nchini.

Nayo, Familia  ya Jango Master ikiwakilishwa na Victor Jango imekubali kulipa fidia hiyo kwa wakati, huku Malulu Ole Moringo naye akiridhia kupokea fidia hiyo kama Serikali ilivyoelekeza.

NYONGO AZITAKA ASASI ZA KIRAIA KUFANYA MAJADILIANO YA PAMOJA ILI KUFANIKISHA DIRA YA MAENDELEO 2050.

NYONGO AZITAKA ASASI ZA KIRAIA KUFANYA MAJADILIANO YA PAMOJA ILI KUFANIKISHA DIRA YA MAENDELEO 2050.

DKT.BITEKO AIPONGEZA TPDC KWA UJENZI WA VITUO VYA CNG.

DKT.BITEKO AIPONGEZA TPDC KWA UJENZI WA VITUO VYA CNG.

DKT.BITEKO ATOA WIKI MOJA KWA TANESCO KUBORESHA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA.

DKT.BITEKO ATOA WIKI MOJA KWA TANESCO KUBORESHA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA.

Mitungi 19,530 kuuzwa kwa bei ya ruzuku kwa lengo la kuhamasisha na kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia

Mitungi 19,530 kuuzwa kwa bei ya ruzuku kwa lengo la kuhamasisha na kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia

NECTA:WALIOFELI KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE KURUDIA DARASA.

NECTA:WALIOFELI KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE KURUDIA DARASA.