SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA

Changamoto ya uhaba wa ajira ni kubwa, vijana wengi wasomi wako mtaani wakiwa hawana ajira rasmi.

The Dododma Post
By The Dododma Post
02 Dec 2024
SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA

Hali hii inasababisha nchi kuwa na idadi kubwa ya vijana tegemezi wasioweza kulipa kodi kwa maendeleo yao na ya taifa kwa ujumla.

Kwa kuliona hilo Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imekuja na mpango Mkakati unaolenga kuongeza wigo wa ajira hadi kufikia ajira mpya milioni 1.2 kila mwaka.

Tayari mpango huo umeshaanza kazi, ambapo katika kipindi cha Januari hadi Julai, 2024, tayari zimezalishwa ajira mpya  607,475 nchini.

Hatua hiyo imesaidia  kupunguza changamoto ya  uhaba wa ajira kwa wastani wa asilimia 50.6 ya lengo la uzalishaji wa ajira mpya  kwa Mwaka.

Aidha Serikali imeendelea kuweka Mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji wa nje na ndani ili kuboresha shughuli za uzalishaji katika sekta za Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Uchimbaji Madini, Viwanda na Biashara ili kuongeza wimbi la wawekezaji katika sekta muhimu za kimkakati.

#KAZIINAONGEA

NYONGO AZITAKA ASASI ZA KIRAIA KUFANYA MAJADILIANO YA PAMOJA ILI KUFANIKISHA DIRA YA MAENDELEO 2050.

NYONGO AZITAKA ASASI ZA KIRAIA KUFANYA MAJADILIANO YA PAMOJA ILI KUFANIKISHA DIRA YA MAENDELEO 2050.

DKT.BITEKO AIPONGEZA TPDC KWA UJENZI WA VITUO VYA CNG.

DKT.BITEKO AIPONGEZA TPDC KWA UJENZI WA VITUO VYA CNG.

DKT.BITEKO ATOA WIKI MOJA KWA TANESCO KUBORESHA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA.

DKT.BITEKO ATOA WIKI MOJA KWA TANESCO KUBORESHA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA.

Mitungi 19,530 kuuzwa kwa bei ya ruzuku kwa lengo la kuhamasisha na kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia

Mitungi 19,530 kuuzwa kwa bei ya ruzuku kwa lengo la kuhamasisha na kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia

NECTA:WALIOFELI KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE KURUDIA DARASA.

NECTA:WALIOFELI KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE KURUDIA DARASA.