TRENI YA MCHONGOKO KUSIMAMA KWA SAA SITA NI HUJUMA:TRC | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

TRENI YA MCHONGOKO KUSIMAMA KWA SAA SITA NI HUJUMA:TRC

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limesema kuwa tukio lililotokea Novemba 3,2024 ambalo lilisababisha treni ya mchongoko (EMU) kusimama kwa takribani saa sita ni hujuma zilizohusisha kukatika ama kukatwa kwa nyaya (catenary) zinazochukua umeme kutoka njia ya umeme kupeleka kwenye treni.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
07 Nov 2024
TRENI YA MCHONGOKO KUSIMAMA KWA SAA SITA NI HUJUMA:TRC

Taarifa iliyotolewa leo Novemba 06,2024 na Mkuu wa Kitemgo cha Uhusiano TRC,Fredy Mwanjala imesema taarifa zilizosambaa  kuwa treni hiyo ilizimika kutokana na changamoto za umeme si kweli kwakuwa hakuna treni ya mchongoko iliyopata hitilafu ya kiufundi.

“Tayari baadhi ya wahusika wamekamatwa na hatua stahiki dhidi yao zimeshaanza kuchukuliwa ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo husika,tunawashukuru  wenzetu wa TANESCO kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa,shirika  linauhakikishia umma kuwa hakuna treni  iliyopata hitilafu ya kiufundi,”amesema Mwanjala.

Amesema TRC imeutaka umma  kupuuza taarifa potofu zinazosambazwa na watu mbalimbali na kwamba ukweli ni kuwa tangu kuanza kwa safari ya kwanza ya treni zinazotumia nishati ya umeme Juni 14, 2024 hakujawahi kuwa na changamoto ya umeme.

“Shirika linawakumbusha wananchi kuwa bado tuko kwenye kipindi cha mwaka mmoja cha matazamio, na kama changomoto zozote zinajitokeza, TRC itaujulisha umma kwa uwazi kama siku zote tunavyofanya, na taarifa rasm mtazipata kwenye vyanzo vyetu rasmi na si vinginevyo.,”amesema Mwanjala.

Waziri Ridhiwani Atoa Wito kwa Vijana Kuchangamkia Fursa Zilizopo.

Waziri Ridhiwani Atoa Wito kwa Vijana Kuchangamkia Fursa Zilizopo.

TPDC ,DC CPP na CPTDC ZASAINI MAKUBALIANO UJENZI WA BOMBA LA GESI ASILIA KUTOKA NTORYA HADI MADIMBA.

TPDC ,DC CPP na CPTDC ZASAINI MAKUBALIANO UJENZI WA BOMBA LA GESI ASILIA KUTOKA NTORYA HADI MADIMBA.

TAKUKURU YAWATAKA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA RUSHWA.

TAKUKURU YAWATAKA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA RUSHWA.

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTOA ELIMU YA SHERIA ZA UCHAGUZI SABASABA.

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTOA ELIMU YA SHERIA ZA UCHAGUZI SABASABA.

Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)

Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)