TPDC YATOA IDHINI KWA TAASISI BINAFSI 40 UJENZI WA VITUO VYA CNG. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

TPDC YATOA IDHINI KWA TAASISI BINAFSI 40 UJENZI WA VITUO VYA CNG.

SHIRIKA la maendeleo ya Petrol Nchini TPDC limetoa ufafanuzi wa chanzo cha tatizo la ukosefu wa gasi ya CNG katika kituo chake cha Airport hali iliyopelekea usumbufu mkubwa kwa magari yanayotumia gesi hiyo ambapo chanzo kilikuwa ni hitirafu ya umeme iliyotokea hivyo katika kuhakikisha hali hiyo haijirudii mara kwa mara tayari wameshatoa idhini kwa taasisi binafsi 40 ili kujenga vituo hivyo.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
03 Oct 2024
TPDC YATOA IDHINI KWA TAASISI BINAFSI 40 UJENZI WA VITUO VYA CNG.

SHIRIKA la maendeleo ya Petrol Nchini TPDC limetoa ufafanuzi wa chanzo cha tatizo la ukosefu wa gasi ya CNG katika kituo chake cha Airport hali iliyopelekea usumbufu mkubwa kwa magari yanayotumia gesi hiyo ambapo chanzo kilikuwa ni hitirafu ya umeme iliyotokea hivyo katika kuhakikisha hali hiyo haijirudii mara kwa mara tayari wameshatoa idhini kwa taasisi binafsi 40 ili kujenga vituo hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Octoba 3,2024 Kaimu Mkurugenzi wa biashara ya petroli na gesi Emmanuel Girbert amesema uhitaji wa gesi ya CNG kwa sasa nchini ni mkubwa hivyo miundombinu iliyopo inapaswa kuongezwa ili kukidhi mahitaji.

"Tumeanza kutumia gesi ya CNG miaka ya hivi karibuni na tukiwa na kituo chetu kimoja cha ubungo lakini hivi sasa mahitaji ni makubwa sana kwani mpaka sasa hivi tunavituo vitatu ambapo kituo kimoja ni kituo dada ambacho kinategemea kutuo mama ambacho mfano wa kituo dada ni kile cha Tazara ambacho kinategemea kituo cha Ubungo",Amesema 

Aidha amesema mpaka sasa kuna magari takribani 4500 ya CNG na vituo vilivyopo uwezo wake ni kujaza magari 1200 mpaka 1500 kwa siku.

"TPDC kwa kuona hadha hiyo tukaona sisi wenyewe hatuwezi kulisha uhitaji tumeshirikisha sekta binafsi   ili kuweza kukidhi mahitaji mpaka sasa tumeshatoa idhini kwa kampuni 40 lakini kasi tuliyoitarajia haikuwa hivyo kasi imekuwa ni ndogo",Amesema Gilbert.

Aidha ameongeza kuwa mpango wa TPDC ni kuhakikisha mpaka ifikapo mwisho wa mwaka huu wa fedha kuwa na vituo 13 zaidi ambavyo ni vipya tofauti na hivyo vitatu vilivyopo.

Akizungumzia mradi wa vituo vya kuhamushika(MOBILE CNG STATION) amesema huo ni moja ya miradi waliyokuwa nayo ambapo inahitajika magari sita la kuweza kutoa huduma hiyo hivyo tayari zabuni ilishatangazwa na kampuni nne za wazawa tayari zimejitokeza.

"Huu ni mpango wa muda mrefu kwani mpaka sasa mikoa iliyopitiwa na bomba letu ni mitatu hivyo hivi vituo sita tumevigawa katika mikoa ambapo 3 vitakuwa Dar es salaam,1 Morogoro ma 2 vitakuwa Dodoma kwa kuanzia",Amesema.

Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.

Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.

Balozi Thobias awapongeza waandishi wa habari kwa ushirikiano  katika tukio la kariakoo.

Balozi Thobias awapongeza waandishi wa habari kwa ushirikiano katika tukio la kariakoo.

MPANGO KAZI KUKOMESHA MAUAJI YA WATU WENYE UALBINO WADAU WAIPONGEZA SERIKALI.

MPANGO KAZI KUKOMESHA MAUAJI YA WATU WENYE UALBINO WADAU WAIPONGEZA SERIKALI.

Wachimbaji wa Madini wahimizwa kulipa kodi ya Serikali.

Wachimbaji wa Madini wahimizwa kulipa kodi ya Serikali.

JAFO AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA NA FCC KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI.

JAFO AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA NA FCC KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI.