SERIKALI KULINDA MILIKI BUNIFU ILI ZIWEZE KUSAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO NCHINI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

SERIKALI KULINDA MILIKI BUNIFU ILI ZIWEZE KUSAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO NCHINI.

SERIKALI imesema itahakikisha inalinda miliki bunifu ili ziweze kusaidia kuondoa changamoto ndani ya jamii kwani maendeleo ya uchumi wa nchi yanategemea bunifu hizo.

Sophia kingimali
By Sophia kingimali
09 May 2024
SERIKALI KULINDA MILIKI BUNIFU ILI ZIWEZE KUSAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO NCHINI.

SERIKALI imesema itahakikisha inalinda miliki bunifu ili ziweze kusaidia kuondoa changamoto ndani ya jamii kwani maendeleo ya uchumi wa nchi  yanategemea bunifu hizo.

Akizungumza leo Mei 9,2024  Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya miliki bunifu duniani,kwa niaba ya waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaja Naibu Waziri wa Utamaduni ,Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjumaa amesema serikali imeshaweka mazingira bora na wezeshi katika suala zima la biashara kwa kutumia miliki bunifu.

"Serikali inauhakika miliki bunifu itaondoa changamoto na kuongeza kipato  cha mtu mmoja mmoja nchini hivyo ineweka mazingira wezeshi kwa kutumia bunifu katika biashara",Amesema.

Hata hivyo Naibu Waziri amewaelekeza BRELA kuhakikisha wamiliki Bunifu  wanatambulika Kwa lengo la kuweza kukopeshwa na kunufaika katika kukuza biashara zao.

"Serikali inauwakika kuwa miliki bunifu zitaondoa chagamoto kwa jamii na zitaongeza ukuaji wa uchumi Kwa mtu mmoja mmoja,"alisema Naibu Waziri.

Mwinjuma amesema anatambua kazi nzuri inayofanya na BRELA katika kuwaimarisha wafanyabiashara na wenye makampuni kutekeleza shughuli zao za kimaendeleo.

"Tutahakikisha ifikapo mwaka 2030 kunakuwa na uwiano wa maendeleo duniani kwa kutumia miliki bunifu",amesema.

Amesema Serikali kwakushirikiana na Taasisi nyingine itawezesha ukamilikaji wa  sera ya miliki bunifu ambayo italeta mwanga katika kusimamia mwongozo wa hati miliki Tanzania.

Aidha amesema Maadhimisho hayo yatumike kama fursa ya kujadili na kutoa maoni ambayo yatakayofanyiwa kazi.

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa amesema masuala ya ubunifu yatasaidia kusukuma ghurudumu la maendeleo mbele hivyo wana mpango wa kuanzisha programu ya miliki bunifu katika vyuo vyote nchini lengo ni kuendeleza ubunifu hizo na kuweza kutumika kwa maslahi ya nchi.

Aidha Nyaisa amesema nchi nyingi zinaendelea duniani kwa sababu ya kueneza miliki bunifu sehemu mbalimbali ndani ya nchi zao.

Nae Mwenyekiti wa bodi ya ushauri BRELA Profesa Neema Mboya amesema Maadhimisho hayo ni muhimu kuendelea kusheherekewa nchini kwani yanatoa fursa ya kukutanisha wadau mbalimbali na kuweza kujadiliana,kujifunza na kupata fursa ambazo zitasaidia kukuza bunifu za wabunifu nchini.

Amesema kufuatia maboresho yanayofanywa ndani ya BRELA yamepelekea kupokea wageni wengi kuja kujifunza wakiwemo Burundi pamoja na Sudani kusini.

RC SENYAMULE ATAMANI DODOMA KUWA JIJI LA KIBIASHARA.

RC SENYAMULE ATAMANI DODOMA KUWA JIJI LA KIBIASHARA.

WAMILIKI wa viwanda watakiwa kuhakikisha wanalipa madeni ya wakulima.

WAMILIKI wa viwanda watakiwa kuhakikisha wanalipa madeni ya wakulima.

Wananchi 'wafunguka' barabara za TARURA zinavyowaongezea kipato na kukuza uchumi wao - Kilolo

Wananchi 'wafunguka' barabara za TARURA zinavyowaongezea kipato na kukuza uchumi wao - Kilolo

TADB WAINGIA MAKUBALIANO NA BENKI YA EXIM KUTOA DHAMANA YA MIKOPO KWA MINYORORO YA THAMANI KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI.

TADB WAINGIA MAKUBALIANO NA BENKI YA EXIM KUTOA DHAMANA YA MIKOPO KWA MINYORORO YA THAMANI KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI.