SERIKALI IMETENGA BILIONI 100 KUJENGA VYUO VYA VETA KWENYE HALMASHAURI 63. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

SERIKALI IMETENGA BILIONI 100 KUJENGA VYUO VYA VETA KWENYE HALMASHAURI 63.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kujenga vyuo vya VETA katika Halmashauri 63 kwenye mikoa isiyokuwa na vyuo hivyo kwa ajili ya kutoa fursa kwa vijana kupata elimu ya ufundi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutengeneza ajira ya kujiajili ama kuajiliwa.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
28 Apr 2024
SERIKALI IMETENGA BILIONI 100 KUJENGA VYUO VYA VETA KWENYE HALMASHAURI 63.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kujenga vyuo vya VETA katika Halmashauri 63 kwenye mikoa isiyokuwa na vyuo hivyo kwa ajili ya kutoa fursa kwa vijana kupata elimu ya ufundi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutengeneza ajira ya kujiajili ama kuajiliwa.

Hayo yamesemwa  Aprili 27, 2024  jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti  wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, MNEC Rehema Sombi, wakati wa mahafari ya 18 ya Chuo cha Furahika kilichopo Buguruni Malapa na kufafanua kuwa fedha hizo zinakwenda kwenye Halmashauri 63 katika mikoa isiyo na vyuo hivyo.

“Mimi ni mtoto wa Ilala na niliwaambia mkiwa na jambo lolote niko tayari kushirikiana nanyi kama ambavyo leo, nitaendelea kuwa balozi wenu ili kuunga mkono juhudi ya Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan katika nyanja ya elimu, jambo hili la kutoa elimu bure linatekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025,” amesema.

Kati ka mahafari hayo ya 18, MNEC Sombi amechangia fedha kwa ajili ya kununua cherehani mbili iliyopokelewa na Mwenyekiti wa Vijana, CCM( W ) Ilala, Juma Mizungu, zitazotumika kwa kufundishia wanafunzi wa fani ya ushonaji wanaojiunga na chuo hicho na kuahidi kuwafikia wahisani ili wakisaidie vifaa vya TEHAMA kama vile kompyuta.

MNEC Sombi katika mahafari hayo ametoa wito kwa wahitimu kuzingatia nidhamu wanapokwenda na kuwa na subra wakati wa kusubiri ajira ili wasijiingize katika tabia ovu ikiwemo uhuni na matumizi ta dawa za kulevya zitakazoharibu ndoto zao.

Naye Mkuu wa Chuo hicho Dkt David Msuya, amesema kwa sasa wanaendelea na ujenzi wa chuo chao kilichopo Kinyerezi jijini Dar es Salaam na kuwaomba wahisani kujitokeza ili kumalizia ujenzi huo utakawapunguzia  adha ya kulipa kodi.

“Tunatumia fedha nyingi kwa ajili ya kulipa kodi ambayo wakati tunalipatukiwa na wanafunzi wachache na imekuwa ni changamoto kwetu hivyo tunawaomba wazazi na walezi kuleta vijana wao katika programu hii ya elimu bure itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi,” amesema.

Ameongeza kuwa wanatoa elimu kwa ngazi ya diploma kwa miaka miwili kwa kozi ya hoteli na nyinginezo na kwa msimu ujao unaoanza Mei mwaka huu wataanza kutoa elimu kwa njia ya mtandao online kwa wahitaji na mwanafunzi atafika chuoni hapo kwa ajili ya kufanya mitihani ya mwisho tu.

Pia amempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt Hussein Mwinyi, kutokana na Kamisheni ya Utalii kupokea wanafunzi wa chuo hicho na wengine kuwapa ajira jambo linalosaidia kutimiza ndoto zao vijana wanaotoka chuoni hapo kuondokana na utegemezi na kuwasaidia familia zao.

Chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 2021 na kupatiwa usajili namba na VET/DSM/PR/2021/D169 kikiwa na wanafunzi wawili na hadi sasa kimefanikiwa kutoa vijana zaidi ya 400 katika fani tofauti ambao wamefanya vema na kupata ajira katika hoteli na mashirika mbalimbali nchini na Serikalini.

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEKUA DED MAFIA KASSIM NDUMBO

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEKUA DED MAFIA KASSIM NDUMBO

MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar

Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar

RC MTWARA AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA KWA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.

RC MTWARA AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA KWA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.