Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewakumbusha viongozi wa Afrika kuendelea kuwekeza katika Kilimo Biashara ili kulinusuru bara la Afrika kukumbwa na uhaba wa chakula kwani asilimia 65 ya ardhi Afrika inafaa kwa kilimo.
Kauli hiyo ameitoa Septemba 7, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati akihutubia Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023) mbele ya marais kutoka nchi mbalimbali kujadili juu ya nini kifanyike kuboresha mifumo ya chakula Afrika.
Amesema Jukwaa hilo linatakiwa kuja na suluhu ya changamoto ya chakula na viongozi wa Afrika wanatakiwa kuwa tayari kuhakikisha Afrika inajitosheleza kwa chakula.
"Asilimia 60 ni vijana ambao ni nguvu kazi, sisi viongozi wa Afrika tupo tayari kuondoa aibu ya Afrika ya kuwa walalamikaji tupo tayari kulisha Afrika na duniani kwa ujumla," amesema Dkt. Samia.
Amesema licha ya rasilimali zilizopo, Afrika wamebaki kuwa walalamikaji baada ya kutafuta suluhisho kuelekea njia ya mapinduzi ya uchumi wa kijani.
"Tupo na AGRF washiriki wa maendeleo sekta binafsi wasomi na wataalamu kubadilishana uzoefu, namna ya mnyororo wa thamani ya bidhaa za kilimo na kujadili mipango ya kuimarisha usalama wa Chakula Afrika," amesema.
Amesema, katika kuelekea mageuzi wanayoyataka katika sekta ya kilimo mataifa ya Afrika hayana budi kuweka mipango na mikakati kufikia Afrika wanayoitaka.
Aidha amesema ili kufikia malengo viongozi wa Afrika hawana budi kufanya tathmini ya vipaumbele vyao na kuvioanisha na mahitaji ya sasa katika muktadha wa dunia.
Amesema zaidi ya watu milioni 283 wanalala njaa Barani Afrika hivyo wanatakiwa kutathmini mambo ya muhimu ili kuboresha kilimo kulikomboa bara la Afrika dhidi ya baa la njaa.
Naye Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto amesema ardhi ya kilimo ipo Afrika hivyo mkutano huo wa AGRF ni somo kubwa, Teknolojia na muda vinahitajika ili kuweza kupata chakula cha kutosha kwenye bara la Afrika hata kupeleka Duniani.
"Tunaweza kuchochea biashara ya kilimo kuacha kuwa watu wa kulalamika wakati ardhi tunayo ni suala la kuongeza uzalishaji na kufikiria tunafanyeje wakulima wazalishe zaidi," amesema Rais Ruto.
Amesema katika somo la mkutano huo wa AGRF ni jinsi gani watafanya mabadiliko ili kubadilisha wakulima waweze kuzalisha kwa wingi ili gharama za chakula zipungue barani Afrika.
REA KUSHIRIKIANA NA NJOMBE KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI ZAIDI YA 13,000
TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII
SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima
BALOZI NCHIMBI KUONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA KIBIKI LEO.
RAIS DK.SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI.
SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima
Kuelekea Maadhimisho ya UKIMWI Duniani,Serikali yaeleza ushamiri wa VVU kitaifa kuwa ni asilimia 4.4
BOT YAWATAKA WANANCHI KUKOPA KWENYE TAASISI ZENYE LESENI YA BENKI HIYO.
RAIS DK.SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI.
Kuelekea Maadhimisho ya UKIMWI Duniani,Serikali yaeleza ushamiri wa VVU kitaifa kuwa ni asilimia 4.4