AMANI NDIYO HIFADHI YA MWANADAMU, TUILINDE- VIONGOZI WA DINI | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

AMANI NDIYO HIFADHI YA MWANADAMU, TUILINDE- VIONGOZI WA DINI

Viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali kutoka kwenye Mikoa ya Kanda ya Kaskazini leo Jumatano Oktoba 22, 2025 wameketi pamoja Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro, kwenye semina ya kujadili kuhusu amani kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, wakisisitiza kuwa hakuna haki, uhai na usalama ikiwa Taifa halina amani na amani ndiyo hifadhi kuu ya mwanadamu, wakisisitiza umuhimu wa kulindwa kwake.

The Dodoma Post
By The Dodoma Post
22 Oct 2025

Akizungumza katika semina hiyo  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Sheikh Shaaban Mlewa amesisisitiza kuwa suala la amani katika Taifa si suala la serikali pekee bali ni suala linalohusu jamii yote kwa ujumla na kwamba amani hujengwa kwa jamii kuwa na tabia ya umoja na utulivu na wote kuwa mstari wa mbele kukemea chuki, uongo pamoja na usengenyaji.

"Raia mwema ndiye anayeleta amani kwa wengine na kuitafsiri amani ni kuepuka kila aina ya maudhi iwe ya kimwili au ya maneno na hii inahimiza kujenga imani na utengamano baina ya wananchi wote bila kujali tofauti zao za kidini, kikabila na kisiasa" amesema Sheikh Mlewa.

Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa mkoa wa Arusha Sheikh Shaaban Bin Juma amesisitiza kuwa amani ndiyo hifadhi pekee ya mwanadamu ma viumbe hai wengine, akisema amani iliyopo nchini ni muhimu kila mmoja kuilinda na kuihifadhi, akisisitiza kuwakataa wale wote wenye kufanya vitendo vya kuhatarisha amani hiyo.

Awali katika semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Godfrey Mnzava kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ametoa wito kwa kila mmoja mwenye sifa kujitokeza kwa wingi kupiga kura hapo Oktoba 29, 2025, akiwahakikishia usalama na mazimgira tulivu wakati wote kampeni, wakati wa upigaji kura na hata baada ya zoezi hilo kukamilika.

Viongozi wa dini Kaskazini wahimiza amani kuelekea Uchaguzi Mkuu

Viongozi wa dini Kaskazini wahimiza amani kuelekea Uchaguzi Mkuu

WAHADZABE WA KARATU WAISUBIRI KWA HAMU OKTOBA 29

WAHADZABE WA KARATU WAISUBIRI KWA HAMU OKTOBA 29

89 WAKAMATWA KUJIHUSISHA NA DAWA ZA KULEVYA.

89 WAKAMATWA KUJIHUSISHA NA DAWA ZA KULEVYA.

NECTA:WATAKAOJIHUSISHA NA UDANGANYIFU MTIHANI WA DARASA LA NNE KUCHUKULIWA HATUA.

NECTA:WATAKAOJIHUSISHA NA UDANGANYIFU MTIHANI WA DARASA LA NNE KUCHUKULIWA HATUA.

RC MAKALLA AZINDUA MSIMU WA SHEREHE ZA MILA ZA KIMASAI

RC MAKALLA AZINDUA MSIMU WA SHEREHE ZA MILA ZA KIMASAI