WATU WANNE MBARONI KWA UMILIKI WA SILAHA | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

WATU WANNE MBARONI KWA UMILIKI WA SILAHA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watuhumiwa wanne kwa kosa la kupatikana na silaha aina ya bastola (pisto) bila kuwa na kibali katika wilaya ya Dodoma Mjini na Mpwapwa,Mei 17

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
20 May 2025
WATU WANNE  MBARONI KWA UMILIKI WA SILAHA

Akizungumza katika kituo kikuu cha Central kati Dodoma,Kamanda wa Polisi, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (SACP) George Katabazi, amesema watuhumiwa hao wanaoshikiliwa ni pamoja na Nestory Kimario mwenye umri wa miaka 38 , Thomas pasco maarufu Sigani mwenye umri wa miaka 39 wote wakazi wa mbabala Mkoani Dodoma.

Aidha Jeshi linawashikilia jumla ya watu 57 kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu, ikiwemo wizi, uvunjaji, na umiliki haramu wa silaha, katika msako maalum unaoendelea maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Aidha, watu wengine wawili walikamatwa wakiwa na silaha za kienyeji Wilayani Mpwapwa zinazotumia risasi aina ya shotgun, wakihusishwa na uhalifu katika maeneo mbalimbali.

Katika tukio tofauti lililotokea Mei 18 2025 usiku, maeneo ya Kizota, watuhumiwa wawili walikamatwa wakisafirisha mafuta lita 2,420 bila vibali halali. Mafuta hayo yanahisiwa kuwa ya wizi na uchunguzi wa kina unaendelea.

“Katika operesheni hii, tumefanikiwa pia kuwakamata watuhumiwa 57 wa makosa ya wizi na uvunjaji. Kati yao, 27 tayari wamefikishwa mahakamani, huku 30 wakiendelea kuhojiwa,” alisema SACP Katabazi.

Vifaa mbalimbali vinavyodaiwa kutumika katika uhalifu pia vimekamatwa, ikiwa ni pamoja na runinga 6, redio 7, pamoja na vifaa 30 vingine vya kuvunjia.


SACP Katabazi ametoa wito kwa wananchi wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuhakikisha wanazikabidhi kwa hiari kupitia ofisi za serikali za mitaa au vijiji kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

“Msako bado unaendelea. Tunawaomba wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa sahihi kuhusu watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu au umiliki haramu wa silaha. Ushirikiano wa jamii ni nguzo muhimu katika kulinda amani na usalama,” alisisitiza Kamanda Katabazi

SERIKALI NA WADAU WAENDELEZA MAPAMBANO YA KIJINSIA

SERIKALI NA WADAU WAENDELEZA MAPAMBANO YA KIJINSIA

Siku Ya Utumishi wa Umma, Watumishi Kufanya Maonesho ya Kutambua Mchango na Umuhimu wao Kwenye Jamii.

Siku Ya Utumishi wa Umma, Watumishi Kufanya Maonesho ya Kutambua Mchango na Umuhimu wao Kwenye Jamii.

Vijana Kutoka Kenya Waonywa Vikali Kuacha Kumkejeli Rais Samia Katika Mitandao ya Kijamii

Vijana Kutoka Kenya Waonywa Vikali Kuacha Kumkejeli Rais Samia Katika Mitandao ya Kijamii

Wizara Imetekeleza Mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Milki za Ardhi(LTIP)

Wizara Imetekeleza Mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Milki za Ardhi(LTIP)