

Ujenzi wa nyumba mbili za kisasa kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum (wasiojiweza) katika kata za Kitobo na Minziro, wilayani Missenyi, Mkoani Kagera, umeingia hatua za mwisho.
Nyumba hizo zilizojengwa na Evance Kamenge ambaye ni mchumi na mkulima ni mfano wa kipekee wa msaada wa kijamii unaotolewa kwa moyo wa dhati.
Kamenge, akielezea nia yake ya kujenga nyumba hizi, amesema aliguswa na maisha magumu wanayoishi wakazi wa maeneo hayo ndipo aliamua kuchukua hatua.
Kwa mujibu wa Kamenge nyumba hizo zitakamilika mwishoni mwa mwezi Juni 2025, ambapo zitakabidhiwa kwa walengwa.
Katika juhudi zake za kusaidia jamii, Kamenge amejenga nyumba hizo kutokana na vyanzo vyake vya mapato na kwa ushirikiano na marafiki zake wa karibu ambao ni wadau wa maendeleo.
Aidha amewaomba wananchi wengine kuchukua hatua kama hiyo huku akisisitiza kuwa kusaidia jamii hakuhitaji mtu kuwa kiongozi, bali inahitaji mapenzi ya dhati ya kusaidia wale walio katika mahitaji.
Moja ya wanufaika, kutoka eneo la Minziro akiwemo Biteganya Mbili amemshukuru Kamenge kwa nyumba hiyo ya kisasa yenye vyumba vitatu na kuahidi kuwa ataendelea kumuombea Kamenge kwa mwenyezi Mungu ili amuongezee neema na baraka,
Mdau huyo amewashukuru wadau wengine walioshirikiana katika msaada huo.
Evance Kamenge ni mzaliwa wa kata ya Kanyigo wilayani Missenyi Mkoani Kagera ameonyesha mfano wa kujitolea katika shughuli za maendeleo bila kujali eneo husika.
Hata hivyo Ujenzi wa nyumba hizo unaleta matumaini ya maisha bora kwa walengwa.
Waziri Mkuu Azindua Mfumo wa Kubadilishana Taarifa Serikalini GovESB.
LUKUVI AWASILISHA BUNGENI TAARIFA YA HALI YA DAWA ZA KULEVYA
UDSM YASAINI MAKUBALIANO NA KAMPUNI ZA CHINA KUTOA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI WA CHUO HICHO.
WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA
MAONESHO YA UTALII NA UWEKEZAJI ZANZIBAR; FURSA KWA WANANCHI KUJUA VIVUTIO VYA UTALII VILIVYOPO NGORONGORO
GRAND BUNGE BONANZA KUFANYIKA JUNI 21 2025 HUKU MGENI RASMI AKITARAJIWA KUWA RAIS SAMIA.
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.
MOI YASEMA WAGONJWA WENGI WANAOWAHUDUMIA WANA MATATIZO SUGU.