

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imekamilisha utoaji wa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini 2,733 kuhusu uchukuaji wa sampuli wakilishi na utambuzi wa jiolojia ya maeneo yenye uwepo wa madini,ambapo mafunzo yalifanyika katika mikoa ya Lindi, Morogoro, Geita na Mwanza.
Hayo yameelezwa na
Notka Banteze Mkurugezi wa Huduma za maabara (GST)
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio na mwelekeo wa Taasisi hiyo kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita Machi 27 katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Dodoma.
Aidha amesema GST ilikamilisha utafiti maalumu wa jiolojia, jiofizikia na jiokemia uliofanyika kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo Wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera na kubaini uwepo wa madini ya kaolini.
Aidha Kupata ithibati za njia nyingine mbili za uchunguzi wa sampuli za madini na kufikisha jumla ya njia tatu zenye Ithibati,Njia hizo ni uchunguzi wa sampuli za dhahabu kwa njia ya kemikali (Aqua Regia) na upimaji wa kiwango cha majivu katika makaa ya mawe kwa njia ya tofauti ya uzito (gravimetric).
"Kupatikana kwa ithibati hizo kumekuwa na manufaa mengi kwa Taifa ikiwemo; kupanua wigo wa majibu ya uchunguzi unaofanywa na maabara ya GST mpaka kutambulika kimataifa; kuongezeka kwa idadi ya sampuli zinazoletwa katika maabara ya GST kwa ajili ya uchunguzi, kuongezeka kwa makusanyo yanayotokana na huduma za maabara"
Aidha, baaada ya ukaguzi uliofanyika mwezi machi, 2025 kupitia chombo kinachotoa Ithibati (SADCAS), maabara ya GST imeendelea kukidhi vigezo vya kuendelea kubaki na ithibati kwa kipindi kingine cha miaka mitano mpaka Oktoba, 2029.
Sanjari na hayo Taasisi imefanikiwa kupata kibali cha ajira na kukamilisha taratibu zote za ajira na kuwezesha watumishi 24 katika kada mbalimbali kuajiriwa na kuripoti kazini.
Aidha, katika bajeti ya 2024/2025 Taasisi imepata kibali cha kuajiri watumishi wengine 34, taratibu za ajira zinaendelea katika mamlaka ya ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira.
"Maboresho ya mazingira ya kazi na vitendea kazi yamefanyika kwa kiwango kikubwa, Vitendea kazi na vifaa vya kisasa vilivyonunuliwa katika kipindi husika ni pamoja na:-Mashine za mionzi za XRD na XRF kwa ajili ya uchunguzi wa sampuli za miamba na udongo, tanuru kubwa la kisasa la uchunguzi wa sampuli za dhahabu lenye uwezo wa kuchunguza sampuli 50 kwa mkupuo kwa muda wa saa moja ikilinganishwa na uwezo wa sampuli 16 kwa mkupuo kwa muda wa saa moja kwa tanuru lililokuwepo"
Aidha GST imeshuhudia mafanikio makubwa ambayo ni pamoja na:-Kuongezeka kwa Makusanyo ya ndani kutoka wastani wa shilingi 1,251,428,472.91 mwaka 2021 hadi shilingi 2,394,211,348 mwaka 2023/2024, sawa na ongezeko la asilimia 91.32, Ongezeko hili limepatikana kupitia mageuzi na maboresho mbalimbali ya kiutendaji yaliyofanyika katika kipindi husika ambayo yaliongeza ubora wa huduma zitolewazo na GST.
"Kuongezeka kwa idadi ya sampuli zinazochunguzwa kutoka wastani wa sampuli 19,184 mwaka 2021 hadi sampuli 25,793 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 34.45. Ongezeko hili limetokana na maboresho makubwa ya maabara yaliyofanyika hasa katika ununuzi wa vifaa na mashine za kisasa za uchunguzi wa sampuli"
Aidha GST kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikamilisha utafiti na uchoraji wa ramani ya jiolojia ya visiwa vya Zanzibar (Unguja na Pemba); ikumbukwe kuwa visiwa vya Zanzibar havijawai kufanyiwa utafiti huo wa jiolojia.
"Matokeo ya utafiti huo yamebaini uwepo wa miamba ya chokaa yenye ubora wa kutengeneza saruji, madini tembo (heavy mineral sands), madini ya silica, strontium, vyanzo vya maji ardhi, maeneo yenye vivutio vya utalii wa jiolojia na maeneo hatarishi kwa majanga ya asili ya jiolojia"Ameongeza
Rais Samia Asisitiza Mchujo wa Wagombea Kufanyika Kwa Haki.
Ilani Ya CCM Imeandaliwa Kwa Weledi Mkubwa Kwa Kushirikiana Na Wananchi;RAIS Dkt.Samia
WIZARA YA ARDHI YAJA NA VIPAUMBELE SABA
SERIKALI NA WADAU WAENDELEZA MAPAMBANO YA KIJINSIA
KAPINGA ATAJA VIGEZO VYA ZIADA UPELEKAJI UMEME VITONGOJINI.