DCEA YAZIDI KUVUNJA MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA NCHINI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

DCEA YAZIDI KUVUNJA MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA NCHINI.

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini ( DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi imekamata jumla ya kilo 2,207.56 za dawa sa kulevya na dawa tiba zenye asili ya kulevya katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam na watuhumiwa saba wanashikiliwa kwa kuhusishwa na dawa hizo.

Sophia kingimali
By Sophia kingimali
25 Nov 2024
DCEA YAZIDI KUVUNJA MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA NCHINI.

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini ( DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi imekamata jumla ya kilo 2,207.56 za dawa sa kulevya na dawa tiba zenye asili ya kulevya katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam na watuhumiwa saba wanashikiliwa kwa kuhusishwa na dawa hizo.

Kati ya dawa hizo ambazo zimekamatwa Skanka ni kilo 1,500.6 ,methamphetamine kilo 687.76 ,heroin kilo 19.20 na chupa 10 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Fentanyl.

Akizingumza jana  jijini Dar es Salaam , Kamishina Jenerali wa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo amesema katika Novemba 14 mwaka huu katika Wilaya ya Kigamboni Mtaa wa Nyangwale wamemawakamata watuhumiwa Mohamed Bakari(40) na Sullesh Mhailoh( 36) ambao ni wakazi wa Mabibo wamakamatwa wakiwa na kilo 1350.4 za dawa za kulevya aina ya Skanka.

Amesema dawa hizo zilikuwa zimefichwa ndani ya nyumba aliyopanga mtuhumiwa Mohamed ambayo alinitumia kama ghala la kuhifadhi dawa hizo .Pia dawa nyingine zilipatikana ndani ya gari aina ya Nissan Juke yenye namba za usajili T 534 EJC zikiwa kwa kusambazwa.

Kamishina Lyimo amesema pia tarehe hiyo hiyo katika mtaa wa Pweza Sinza E wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam mtuhumiwa Iddy Mohamed Iddy(46) mkazi wa Chanika Buyuni alikamatwa akiwa na kilo 150.2 za Skanka zilizokuwa zimefichwa katika maboksi ya sabuni

Pia amesema na baadhi ya dawa hizo nyingine zilikuwa zimefichwa kwenye boksi lililotengenezwa kwa bati gumu na kupachikwa katika chassis ya gari aina ya scania lenye namba za usajili wa Afrika Kusini LN87XGP. Gari hiyo imekuwa ikitumika kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi.

Akielezea zaidi amesema Novemba 17 mwaka huu katika Jiji la Tanga watuhumiwa Ally Kassim Ally (52) na Fahad Ally Kassim (36) walikamatwa Mtaa wa Mwakibila wakiwa na kilo 706.96 za dawa za kulevya aina ya heroin na methamphetamine.

Kamishina Jenerali Lyimo amesema baadhi ya dawa hizo zimepatikana ndani ya gari aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T 714 EGX huku nyingine zikibainika kufichwa katika nyumba aliyopanga mtuhumiwa.

Pia amesema Novemba 19 mwaka huu katika Mtaa wa Kupata na Nyamwezi Kariakoo jijini Dar es Salaam watuhumiwa Michael Mziwanda(28) mkazi Tabata Segerea na Tumpale Mwasakila(32) Mkazi wa Temeke Mikoroshini walikamatwa na chupa 10 za dawa zenye asili ya kulevya aina ya Fentanyl wakiwa nazo katika duka la M-Pesa .

Aidha katika opresheni hizo zilizofanyika wamekamata magari matatu na boti moja ambavyo vimekuwa vikitumika katika uhalifu na viko chini ya ulinzi.

"Dawa zilizokamatwa ni nyingi na zingeweza kuwa na madhara makubwa kwa jamii na Taifa ikiwa zingeingia mitaani.Dawa hizi haziathiri tu wale waliokwishaanza matumizi ya dawa za kulevya bali pia wafanyabiashara hawa wa dawa hulenga watu wengine ambao hajaanza matumizi ili kutanua masoko yao.

MENEJIMENTI YA MOI YAWAPA ZAWADI NA SHUKURANI WATUMISHI WAKE

MENEJIMENTI YA MOI YAWAPA ZAWADI NA SHUKURANI WATUMISHI WAKE

Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.

Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.

Balozi Thobias awapongeza waandishi wa habari kwa ushirikiano  katika tukio la kariakoo.

Balozi Thobias awapongeza waandishi wa habari kwa ushirikiano katika tukio la kariakoo.

MPANGO KAZI KUKOMESHA MAUAJI YA WATU WENYE UALBINO WADAU WAIPONGEZA SERIKALI.

MPANGO KAZI KUKOMESHA MAUAJI YA WATU WENYE UALBINO WADAU WAIPONGEZA SERIKALI.

Wachimbaji wa Madini wahimizwa kulipa kodi ya Serikali.

Wachimbaji wa Madini wahimizwa kulipa kodi ya Serikali.