WAZIRI wa Maliasi na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana amesema onesho la Swahili International Tourism Expo S!te kwa mwaka huu limekuwa na mafanikio makubwa kwani limeingiza takribani wanununuzi 120 wa Kimataifa wa bidhaa za utalii.
WAZIRI wa Maliasi na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana amesema onesho la Swahili International Tourism Expo S!te kwa mwaka huu limekuwa na mafanikio makubwa kwani limeingiza takribani wanununuzi 120 wa Kimataifa wa bidhaa za utalii.
Hayo ameyasema leo Octoba 13,2024 wakati akifunga Onesho la Swahili International Tourism Expo (S!TE) mwaka 2024 Jijini Dar es Salaam amesema mafanikio hayo makubwa yamechagizwa na uwepo wa filamu ya The Royal Toure iliyofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
"Mwitikio huu mkubwa tuliouona na kuliosababisha Onesho hilo kuwa na idadi kubwa ya
washiriki ni pamoja na filamu ya The Royal Toure aliyofanywa na Rais Dkt Samia imepelekea watalii wengi kuja nchini na kujionea vivutio vilivyopo",Amesema.
Amesema sekta ya Utalii imekuwa ikichangia Kwa kiasi kikubwa Pato la Taifa kwani mtalii kuanzia anashuka airport,tax anayochukua na hoteli anayofikia pamoja na kule anakotembelea kote anaacha fedha za kigeni ambazo huchangia Pato la Taifa.
Aidha ameongeza kuwa Ulinzi wa rasilimali za nchi ikiwemo Misitu na mbuga ni muhimu sana Kwa Taifa na kipaumbele hivyo kila mtu anapaswa kuilinda ili kuendelea kustawisha uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania,Balozi Dr Ramadhan Dau amesema mafanikio waliyopata Kwa mwaka huu ni ishara tosha ya mafanikio ya maandalizi ya Onesho lijalo ambapo Kwa mwaka huu limefanyika Kwa mara ya nane tangu lilipoanzishwa mnamo mwaka 2014.
Naye Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Misitu Nchini (TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema Utalii wao kwa kiasi kikubwa upo kwenye Mazingira Ikolojia ambayo ni ya kuona na kuushughulisha mwili na akili hususani kwenye masuala ya kutembea kwenye Misitu, kupumzika, kupanda milima na michezo mbalimbali .
Aidha amesema kuwa fursa hizo zikitumika vizuri zitawafanya watalii kukaa kwa mda mrefu zaidi Tanzania hivyo kuongeza Pato la taifa na uchumi wa watanzania utakua.
Aidha amewataka watanzania kushiriki katika kuhifadhi Maliasili za Tanzania ikiwemo Misitu ambayo inasaidia kunatunza mazingira na kuleta hewa Safi.
MPANGO KAZI KUKOMESHA MAUAJI YA WATU WENYE UALBINO WADAU WAIPONGEZA SERIKALI.
Wachimbaji wa Madini wahimizwa kulipa kodi ya Serikali.
JAFO AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA NA FCC KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI.
JAMII YAASWA KUTUMIA NISHATI SAFI ILI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA MHE.RAIS
FDH YAIPONGEZA UNEP KUENDELEZA AGENDA YA MAZINGIRA KWA WENYE ULEMAVU
JAMII YAASWA KUTUMIA NISHATI SAFI ILI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS SAMIA
THE WHEEL YALETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI NCHINI.
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.
FDH YAIPONGEZA UNEP KUENDELEZA AGENDA YA MAZINGIRA KWA WENYE ULEMAVU