

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), Shadrack Mziray amezitaka halmshauri nchini kuweka utaratibu bora utakaohakikisha miradi ya kunusuru kaya maskini inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali inakamilika kwa wakati.
Mziray ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete katika ziara yake ya kikazi mkoani Njombe. Mtendaji huyo wa Tasaf yupo mkoani Njombe kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali za miradi inayotekelezwa na taasisi hiyo.
"Kwa hii miradi iliyopelekewa fedha, mkurugenzi lazima muweke msisitizo su utaratibu maalumu utakaonyesha baada ya muda fulani miradi ya Tasaf inakamilika," amesema
"Kuweni na mkakati mahsusi wa kuhakikidha hii miradi ya Tasaf inayoendelea na iliyopata fedha inakamilika kwa wakati chambueni changamoto za kila mradi mmoja mmoja ili kujua namna ya kuzitatua kulingana na mkakati wetu," amesema Mziray.
Mziray amesema kuna dhana iliyojengeka kwamba miradi ya Tasaf lazima inatekelezwa ndani ya miezi 12, jambo ambalo siyo sahihi bali hata ndani ya miezi minne inaweza kukamilika kama ilivyo mingine ikiwemo ua uboreshaji wa elimu.
" Mingine inakamilika ndani ya miezi mitatu kwa nini Tasaf isiwe hivyo? Ambayo fedha yake inakuja yote," amesema Mziray.
Mziray aliutaka mkoa wa Njombe kukamilisha kwa wakati miradi ya Tasaf ikiwemo wa miundombinu, inayotekeleza katika wilaya mbalimbali ikiwemo ya Makete akishauri kuweka mkakati ili miradi yote ikamilike kwa wakati ili kurahisisha huduma kwa wananchi.
"Tasaf tupo tayari kushirikiana na nyie (mkoa wa Njombe) ili kuhakikisha miradi inakamilika," amesema Mziray.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Makete William Makufwe amesema kuna baadhi ya miradi imekamilika na mingine inaendelea kufanyiwa kazi, akiushuruku uongozi wa Tasaf makao makuu kwa ushirikiano wao katika utekelezaji wa miradi hiyo.
"Timu ya wilaya ya Makete tunafanya vizuri kwa ushirikiano katika utekelezaji wa miradi hii, na maeneo mengi tulipata fedha za nyongeza ya utekelezaji wa miradi hasa ya ujenzi," amesema Makufwe.
BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.
SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.
DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.
ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC
VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI