

Matukio mbalimbali Mkoani Rukwa ambapo wananchi wamejikusanya kumshuhudia Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye leo tarehe 16 Julai 2024 anatarajiwa kuzindua vihenge na maghala ya kisasa ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), katika eneo la Kanondo, Mkoani Rukwa
Matukio mbalimbali Mkoani Rukwa ambapo wananchi wamejikusanya kumshuhudia Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye leo tarehe 16 Julai 2024 anatarajiwa kuzindua vihenge na maghala ya kisasa ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), katika eneo la Kanondo, Mkoani Rukwa.
Kukamilika kwa Mradi huo kumewezesha NFRA kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka za aina tofauti kama vile mahindi, mtama na mpunga katika Mkoa wa Rukwa kutoka tani 33,500 hadi tani 58,500; kwa maana ya ongezeko la vihenge tani 20,000 na maghala tani 5,000.
Maghala hayo ya kisasa yana mfumo mzuri wa kupitisha hewa ambao pia unaoruhusu ufanisi katika uhudumiaji mazao (improved ventilation sytem and improved logistical system); ikiwa ni pamoja na utumiaji wa zana mbalimbali za kazi (matrekta, mizani, elevators).
Mradi huo ulianza mwezi Julai 2019 na umegharimu Dola za Marekani milioni 6,019,000 sawa na takribani shilingi bilioni 14. NFRA inaendelea kujipanga kuongeza uwezo wa teknolojia ya vihenge na maghala ili kuendana na uzalishaji wa chakula hapa nchini.
#KilimoNiBiashara
#TwenzetuShambani
Maiko Salali Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mpwapwa, Apongeza CCM kwa Ujumuishwaji wa Makundi Maalum
DIB YAHIMIZA WANANCHI KUDAI FIDIA ZAO KUTOKA BENKI ZILIZOFILISIKA
USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA
DWIGHT DANDA KIJANA MDOGO NA MHITIMU WA CHUO KIKUU ATIA NIA UBUNGE KIBAMBA
BoT YAWATAKA TAMFI NA TAMIU KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA.
Aliyeongoza kura maoni Vunjo 2020, kumkabili tena Dkt. Kimei
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake
Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma