

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati, Falician Mramba, ameipongeza, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa majukumu wanayoetekeleza.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati, Falician Mramba, ameipongeza, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa majukumu wanayoetekeleza.
Amesema wanahakikisha udhibiti wa bei ya bidhaa, huduma yenyewe inapatikana na kudhibiti ubora wa huduma.
Hayo ameyasema Leo Julai 9,2024 wakati alipotembelea banda la EWURA katika Maoneshoa ya 48 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es salaam.
Amesema kuhusu udhibiti wa bei ya bidhaa, Tanzania ni nchi ambayo bei za nishati ya umeme zipo chini zaidi.
"Nchi yetu ni yenye bei ya chini ya umeme, hata ukilinganisha na nchi majirani zetu utabaini hili.
"Kadhalika aupatikanaji wa huduma hii umeimarika sana, hatusemi kwamba ubora umetulia mahali ambapo hamna shida, hapana ila angalau tupo kwenye ubora mzuri," amesema.
Kuhusu gesi asilia amesema wanafanya vizuri kutoa leseni kwa wale wanaotaka kuchimba visima ili jamii inufaike.
Amesema serikali inaendelea kuisimamia vyema mamlaka hiyo ili itekeleze vyema majukumu yake.
Amesema pia zipo huduma za kiushauri na malalamiko ambazo EWURA wanatoa kwa wananchi ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa EWURA, Dkt. James Andilile ameahidi kuwa wataendelea kuhakikisha huduma wanazotoa za umeme na gesi asilia zinaendelea kupatikana katika ubora unaotakiwa.
Amesema pia kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya uwekezaji na mwezi uliopita walitiana saini ya kupimana utendaji kazi.
Amesema pia wanatekeleza majukumu mbalimbali ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya umeme hususani Mradi wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere.
Kwa upande wa sekta ya mafuta, amesema wanaendelea kufuatilia ubora wa mafuta na hadi Juni 30 habari ya ubora wa mafuta ulikuwa umefikia asilimia 97.
Amesema lengo ni kuhakikisha mafuta yanauzwa kwenye ubora unaotakiwa na kufuatilia mwenendo wa bei za soko la dunia ili kuangalia unafuu wa bei kwa wananchi.
Ameahidi kuendelea kutoa bei za kila mwezi na kwamba wamegeukia pia gesi ya kwenye magari na kuwapo kwake kumesaidia kupunguza matumizi ya Dola nchini kwasababu huduma hiyo inapatikana Tanzania.
Kuhusu sekta ya maji amesema wanaendelea kufuatilia upatikanaji wa huduma na kila eneo serikali inafanya uwekezaji ambao utasaidia kuwa na huduma za kutosha.
"Jukumu letu ni kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za maji kila sehemu," Amesema.
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA TANGA YATOA ONYO KWA WATU WANAOPANGA KUVUNJA AMANI SIKU YA UCHAGUZI
JIJI LA DAR ES SALAAM NI SHWARI,JITOKEZENI KUPIGA KURA:RC CHALAMILA.
VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA WATANZANIA KUPIGA KURA KWA AMANI.
BODABODA NA MACHINGA HATUTAKUWA CHANZO KUVUNJA AMANI YETU
CWT YATOA WITO KWA WALIMU KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU NA KUELEIMISHA JAMII KUHUSU UMUHIMU WA KUPIGA KURA
PADRI NIKATA ALIJIPOTEZA KUTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO NA KUACHWA NA MPENZI WAKE- POLISI
BRIGEDIA JENERALI NDAGALA AFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA USIMAMIZI WA MAAFA JIJINI MBEYA
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
MKURANGA WAPO TAYARI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU KWA AMANI
Vijana sasa kujifunza ufundi kwa urahisi kupitia programu ya VSOMO ya VETA