

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson amezindua mbio za Bunge Marathon Aprili 13,2024 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma lengo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga Shule ya Sekondari ya Wavulana.
Mbio hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya, Waheshimiwa Wabunge na Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi pamoja na wadau wa michezo.
Akizungumza kwenye bonanza hilo Spika Tulia ameeleza kufurahishwa kwake na ushiriki wa wazee, walemavu na watoto waliojitokeza kukimbia mbio za kilometres tano hadi kilometers 10 na kueleza kuwa huo ni uzalendo unaofaa kuigwa.
Mbali na kufurahishwa na ushiriki huo ametumia nafasi hiyo kuitaka jamii kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuipunguzia mzigo serikali wa magonjwa yasiyo ambukizwa.
"Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kupambana na magonjwa hayo, jamii inapaswa kuthamini michezo,nimefurahishwa na mzee wa Miami 92 kukimbia mbio za kilometres 10 huku watoto kuanzia umri wa miaka 5 hadi 9 kukimbia mbio za kilometres 5 hongereni Sana kwa kujitoa kwenu, "amesema
Sambamba na hilo amesema marathon hiyo inalenga kuchangia ujezi wa shule ya secondary ya wavulana ambapo kila mbunge atachangia shilingi Million 3.5 huku akibainisha kwa kila mchangiajiajina yao yataandikwa kwa wino wa dhahabu na kihifadhiwa shuleni hapo
Mbio hizo za kuanzia Km 21, Km 10 na Km 5 zimeongozwa na wadau mbalimbali wakishiriki wakiwemo Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake Meya wa Jiji la Dodoma Devis Mwamfupe amesema michezo ni furaha na huleta amani huku akimshukuru Spika wa Bunge kwa kuwa na maono ya kuwagusa Wavulana.
Maiko Salali Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mpwapwa, Apongeza CCM kwa Ujumuishwaji wa Makundi Maalum
DIB YAHIMIZA WANANCHI KUDAI FIDIA ZAO KUTOKA BENKI ZILIZOFILISIKA
USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA
DWIGHT DANDA KIJANA MDOGO NA MHITIMU WA CHUO KIKUU ATIA NIA UBUNGE KIBAMBA
BoT YAWATAKA TAMFI NA TAMIU KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA.
Aliyeongoza kura maoni Vunjo 2020, kumkabili tena Dkt. Kimei
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake
Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma