

Dodoma.Serikali kupitia Wizara ya Afya imepanga kuendelea kutoa chanjo kwa watoto zaidi ya milioni tano ya ugonjwa wa Saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa mabinti wa miaka tisa hadi kumi na nne ili kuwakinga na vimelea vya ugojwa huo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha elimu ya Afya kwa umma Dkt Tumaini Haonga jana tarehe 12 Aprili, 2024 wakati wa semina ya waandishi wa habari kuhusu chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi jijini Dodoma.
Haonga amesema kuwa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi itatolewa kwa dozi moja, ambapo awali ilikuwa ikitolewa kwa watoto wenye umri wa miaka kumi na minne tu kwa dozi mbili.
“Kufuatia tafiti ya WHO na kwa kuzingatia mingozo ya wizara yetu ya afya imeona chanjo ya HPV inaweza kuwa na ufanisi wa kutosha kwa kumkinga mtoto kutokana na vimelea vya saratani ya mlango wa kizazi hata kwa dozi moja, ambapo awali tulikuwa tunawapatia dozi mara mbili, nitoe rai kwa watanzania kuwatoa watoto hao ili kuweza kupatiwa chanjo hii”. Amesema Dkt. Haonga.
Aidha, Dkt. Haonga amevitaka vyombo vya habari kote nchini kutumia taaluma zao kuhamasisha, kuelimisha na kuwapa ufafanuzi wananchi juu ya masuala mazima ya afya hususani kuhusu ugonjwa huo kwa sababu wananchi wengi wanategemea kupata taarifa kupitia vyombvo vya habari.
“Nitoa wito kwa wanahabari kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha taarifa, elimu na uhamasishwaji wa jamii kuhusu chanjo hii zinawafikia watanzania, ninyi wanahabari mna vyanzo vingi vinavyoweza kuwafikia watanzania kwa wingi hivyo mkatoe taarifa kuhusu afya ili kufikia dhima ya Serikali ya kuwakinga wananchi na saratani ya mlango wa kizazi na kuhakikisha tunakuwa na taifa zenye afya bora”. Amesisitiza Dkt. Haonga.
Pia amewataka watanzania wote kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara ili kuwahi kuchukua hatua stahiki pindi wanapobainika kuwa wana changamoto ya ugonjwa.
Awali akitoa wasilisho Afisa Progamu wa Mpango wa Taifa wa Chanjo Bi. Lotalis Gadau amesema lengo la kampeni ya chanjo ya saratani ya kizazi ni kuwapa kinga mabinti wa miaka tisa hadi kumi na nne na kuzuia kuenea kwa maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake hapo baadae.
“Tunalenga kuwapatia mabinti wenye umri wa miaka tisa hadi kumi na nne kwa sababu wanakuwa hawajaanza kujamiana ili kumkinga na virusi vya saratani ya mlango wa kizazi kwa sababu virusi hivyo vinaambukizwa kwa njia ya kujamiana na mmoja ya athari ya ungonjwa huu usipogundulika mapema ni kifo”. Amesema Bi. Gadau.
Aidha Gadau amesema kuwa inakadiriwa kwamba takribani wanawake zaidi ya elfu kumi wanapata saratani ya mlango wa kizazi kila mwaka na wanawake zaidi ya elf sita hupoteza maisha pia amewahasa wanawake na mabinti kufanya vipimo vya saratani ya mlango wa kizazi ili kujua afya zao mapema.
Maiko Salali Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mpwapwa, Apongeza CCM kwa Ujumuishwaji wa Makundi Maalum
DIB YAHIMIZA WANANCHI KUDAI FIDIA ZAO KUTOKA BENKI ZILIZOFILISIKA
USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA
DWIGHT DANDA KIJANA MDOGO NA MHITIMU WA CHUO KIKUU ATIA NIA UBUNGE KIBAMBA
BoT YAWATAKA TAMFI NA TAMIU KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA.
Aliyeongoza kura maoni Vunjo 2020, kumkabili tena Dkt. Kimei
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake
Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma