PIC YAIPONGEZA TRC KWA UBUNIFU. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

PIC YAIPONGEZA TRC KWA UBUNIFU.

KAMATI ya Bunge ya Kudumu ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PIC) imepongeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa ubunifu waliouonesha wa kuwezesha kuongeza mapato ya nchi nje ya mfumo mzima wa uendeshaji wa reli.

Sophia kingimali
By Sophia kingimali
27 Mar 2024
PIC YAIPONGEZA TRC KWA UBUNIFU.

KAMATI ya Bunge ya Kudumu ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PIC) imepongeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa ubunifu waliouonesha wa kuwezesha kuongeza mapato ya nchi nje ya mfumo mzima wa uendeshaji wa reli.

Kauli hiyo ilitolewa leo March 27,2024 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deus Sangu baada ya kamati hiyo kukagua utekelezaji wa mradi wa Reli ya Kisasa ya Kimataifa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro.

Sangu alisema ujenzi huo unaonesha kuwa na manufaa mengi kwa kuwa TRC wanao mpango wa kutumia maeneo mengine kutoa huduma nyingine zikiwemo za kibenki na simu.

" Tunampongeza ubunifu huo kwani utachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza mapato ya serikali,"amesema.

Akitoa majumuisho ya kamati hiyo

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo  Augustino Vuma amesema 

kupitia mradi wa SGR kazi kubwa imefanyika ni kweli serikali imefanya Uwekezaji mkubwa na  imerudhishwa na mradi huo Kwa sababu imetekelezwa katika viwango vinavyostahili.

"Tumefurahishwa kusikia mradi huo kuwa umetengeneza ajira rasmi 30,000 ambazo zimewezesha upatikanaji wa kiasi cha sh. bilioni 350.

"Tunaamini Watanzania watatumia muda mfupi kusafiri na gharama za mizigo zitapungua kwa asilimia 40," amesema.

Amesema gharama za mradi ni sh.trilioni 23.3 na asilimia 40 ya fedha hizo serikali imeshatoa hivyo ameitaka TRC kuendelea kutunza miundombinu ya mradi huo na kuwasimamia wakandarasi kukamilisha vipande vilivyosalia ili mradi huo ianze Kwa muda unaotarajiwa.

Pia amewataka Watanzania kuhakikisha wanatumia fursa za mradi huo katika kukuza kipato chao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TRC, Ali Karavina amesema Shirika litaemdelea kutekeleza maelekezo ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.

"Kuhusiana na bei ya nauli ya treni ya SGR zinashughulikiwa na Mamlaka husika na kabla ya kuanza safari Julai, mwaka huu Kila kitu kitakuwa wazi,"amesema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa amesema Kamati ya PIC ni muhimu kwa taasisi na Shirika hilo limekuwa likichukua fedha nyingi katika bajeti ya serikali kuliko taasisi zingine.

"Tunashukuru sana Kamati ya Bunge ya PIC tunaahidi kuchapa kazi ili Julai tuanze safari za Dar es Salaam-Dodoma,"amesema

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEKUA DED MAFIA KASSIM NDUMBO

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIYEKUA DED MAFIA KASSIM NDUMBO

MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar

Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ya Zanzibar

RC MTWARA AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA KWA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.

RC MTWARA AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA KWA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.