Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tanga imetoa onyo kali kwa wananchi wote wenye nia ovu ya kuvunja amani katika kipindi cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, ikisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayejihusisha na vitendo hivyo.

Onyo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Buriani, wakati akizungumza na waandishi wa habari akiwa ameambatana na Kamati ya Amani pamoja na viongozi wa vyama vya siasa mkoani humo.
Balozi Batilda amesema serikali haitasita kuchukua hatua kwa mtu yeyote atakayehatarisha utulivu na amani ya mkoa huo siku ya uchaguzi.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani na kuacha kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani.
Kamati hiyo imewahakikishia wananchi kuwa maandalizi yote muhimu kwa ajili ya uchaguzi yamekamilika, na imewataka wakazi wa Tanga kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo kwa utulivu na nidhamu.
89 WAKAMATWA KUJIHUSISHA NA DAWA ZA KULEVYA.
NECTA:WATAKAOJIHUSISHA NA UDANGANYIFU MTIHANI WA DARASA LA NNE KUCHUKULIWA HATUA.
MRADI WA HEET WAFUNGUA UKURASA MPYA WA MAGEUZI KATIKA ELIMU NCHINI.
WANNE JELA MIAKA SABA KWA JARIBIO LA KUMTEKA MFANYABIASHARA
Kilimo Ni Mhimili wa Uchumi wa Tanzania Kikichangia Asilimia 26.5 ya Pato la Taifa.
PADRI NIKATA ALIJIPOTEZA KUTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO NA KUACHWA NA MPENZI WAKE- POLISI
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
WANNE JELA MIAKA SABA KWA JARIBIO LA KUMTEKA MFANYABIASHARA
Vijana sasa kujifunza ufundi kwa urahisi kupitia programu ya VSOMO ya VETA
CHALAMILA: WATAKAOJIZIMA DATA OKTOBA 29, TUTAWAFANYA NETWORK ZISOME