

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, amesema kuwa uchaguzi wa amani na bila vurugu unawezekana endapo kila Mtanzania atazingatia sheria, taratibu na maadili ya kitaifa wakati wa kipindi cha kampeni na upigaji kura.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, amesema kuwa uchaguzi wa amani na bila vurugu unawezekana endapo kila Mtanzania atazingatia sheria, taratibu na maadili ya kitaifa wakati wa kipindi cha kampeni na upigaji kura.
Akizungumza jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), tukio lililokwenda sambamba na uwasilishwaji wa Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima kwa mwaka 2024, Dkt. Mkuya aliwakumbusha wananchi umuhimu wa kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha na mali zao
“Ni muhimu Watanzania wakatambua kuwa amani ni msingi wa maendeleo. Uchaguzi unaweza kufanyika kwa utulivu bila vurugu, bila chuki na bila madhara. Tukiwa watiifu kwa sheria, hatutalazimika kukabiliana na majanga ambayo hata bima haziwezi kulipia madhara yake kwa sababu ni ya kujitakia,” alisema Dkt. Mkuya.
Aidha, Waziri huyo alitumia fursa hiyo kupongeza TIRA kwa jitihada kubwa za kusimamia sekta ya bima nchini, akisisitiza kuwa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa bima ni nyenzo muhimu ya kujenga uchumi imara na jamii yenye uelewa wa kifedha.
CWT YATOA WITO KWA WALIMU KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU NA KUELEIMISHA JAMII KUHUSU UMUHIMU WA KUPIGA KURA
JWTZ NA POLISI MOROGORO WAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KUJIIMARISHA KATIKA ULINZI NA USALAMA
Hakuna Maendeleo Bila Amani, Hakuna Taifa Imara Bila Mshikamano - Dkt. Judith
VIONGOZI WA DINI KATAVI WATOA KAULI "UCHAGUZI USITUGAWANYE"
WOTE WENYE HOMA ZA UCHAGUZI MSIKUBALI ZIKAPANDA KICHWANI, TUTAWADHIBITI- KANALI MTAMBI
PADRI NIKATA ALIJIPOTEZA KUTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO NA KUACHWA NA MPENZI WAKE- POLISI
BRIGEDIA JENERALI NDAGALA AFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA USIMAMIZI WA MAAFA JIJINI MBEYA
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
MKURANGA WAPO TAYARI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU KWA AMANI
Vijana sasa kujifunza ufundi kwa urahisi kupitia programu ya VSOMO ya VETA