WAANDISHI WA HABARI DODOMA WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA NA ULINZI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

WAANDISHI WA HABARI DODOMA WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA NA ULINZI.

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (Dodoma Press Club) wamepatiwa mafunzo ya usalama wa kimwili, kidijitali na afya ya akili, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kujilinda binafsi katika mazingira ya kazi.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
18 Aug 2025
WAANDISHI WA HABARI DODOMA WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA NA ULINZI.

Mafunzo hayo yalifanyika Agosti 16, 2025, yakiongozwa na Mkufunzi wa Usalama na Ulinzi, Okuly Julius, ambaye pia ni mwandishi wa habari. Okuly alipata mafunzo hayo kupitia Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na kisha kupewa jukumu la kuwajengea uwezo waandishi wenzake katika mikoa.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo, Okuly amesema waandishi wa habari wanapaswa kuwa makini na kuchukua tahadhari muda wote kwani usalama huanzia kwa mwandishi mwenyewe.

“Ni muhimu kuchukua tahadhari kubwa dhidi ya mashambulizi ya kimtandao kwa kuhakikisha viunganishi vinavyopokelewa vinathibitishwa kabla ya kubofya, kutumia nywila imara na kuweka uthibitishaji wa hatua mbili. Waandishi wanapaswa kuwa makini zaidi hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, kipindi ambacho mara nyingi huambatana na vitisho, ukatili na hata kukamatwa kiholela,” alisema Okuly.

Ameongeza kuwa ni vyema waandishi kutoa taarifa kwa watu wa karibu au wenzao wanapokwenda kwenye kazi, ili kuepuka hatari zinazoweza kutokea endapo watapatwa na matatizo wakiwa peke yao.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Bahati Msanjila (Crown Media), Saida Issa (Gazeti la Zanzibar Leo), Rhoda Simba (Channel Ten), Gideon Gregory (Jambo FM) na Joyce Kasiki (Gazeti la Majira), walisema yamewajengea uwezo mkubwa na sasa wanafahamu mbinu bora za kufanya kazi kwa usalama.

Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa “Empowering Journalists for Informed Community” (Kuwawezesha Waandishi wa Habari ili Jamii Iweze Kupata Taarifa Sahihi) unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC). Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano wa International Media Support (IMS), Union of Tanzania Press Clubs (UTPC) na JamiiAfrica.

KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI  MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA

KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.

TANZANIA KUWA KINARA WA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIMAABARA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

TANZANIA KUWA KINARA WA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIMAABARA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

MWENYEKITI CCM  RAIS  DKT.SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU.

MWENYEKITI CCM RAIS DKT.SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU.

JAJI MUTUNGI AVITAKA VYAMA VYA SIASA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU KULINDA AMANI YA NCHI.

JAJI MUTUNGI AVITAKA VYAMA VYA SIASA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU KULINDA AMANI YA NCHI.