JAJI MUTUNGI AVITAKA VYAMA VYA SIASA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU KULINDA AMANI YA NCHI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

JAJI MUTUNGI AVITAKA VYAMA VYA SIASA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU KULINDA AMANI YA NCHI.

Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vya siasa kufanya kampeni za kistaarabu na kujiepusha kutoa lugha zitakazopelekea kuvunja amani ya nchi.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
18 Aug 2025
JAJI MUTUNGI AVITAKA VYAMA VYA SIASA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU KULINDA AMANI YA NCHI.

Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vya siasa kufanya kampeni za kistaarabu na kujiepusha kutoa lugha zitakazopelekea kuvunja amani ya nchi.

Wito huo ameutoa leo Agosti 18,2025 wakati akifungua mafunzo ya siku moja kuhusu sheria ya gharama za uchaguzi kwa viongozi wa vyama vya siasa ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea uchaguzi mkuu octoba 2025.

Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa wa  kutekeleza sheria hiyo hivyo amewataka kusikiliza na kuoelewa vizuri ili waweze  kuwa mabalozi wazuri kwa wengine.

"Nipende kuwakumbusha ndugu zangu vyama vya siasa kuna maisha baada  ya Uchaguzi  hivyo Amani ya Taifa ipiwe kipaumbele  katika  Uchaguzi huu nchi ikingia kwenye machafuko hatukuwa na siasa wala amani hivyo tuwe mabalozi wa amani," amesema

Hata hivyo Jaji Mutungi amewataka viongozi hao waendelee kurithisha amani iliyo tengenezwa na waasisi wa Taifa kwa vizazi vijavyo.

Sambamba na hayo Jaji Mutungi amewasisitiza wagombea  wahakikishe wanakuwa na sera nzuri zitakazowafanya wananchi wawachague lakini si kutumia lugha za matusi dhidi ya chama kingine pindi watakapokuwa wanafanya kampeni zao.

Pia amewataka viongozi hao kuwa makini na taarifa wanazozikuta mitandaoni ambazo hazina ukweli ambazo zinapelekekea sintofahamu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi  

"Viongozi tunatakiwa kuwamakini sana kipindi hiki  unaweza ukaamka asubuhi ukaona taarifa za uvumi zinasema hakuna Uchaguzi hivyooo tuupuze Uchaguzi  upo na Uchaguzi utakuwa wa amani na haki,"amesema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Juma Khatibu, amewataka viongozi na watendaji wa vyama vya siasa nchini kuzingatia kwa makini masharti ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi ili kuepusha dosari na kasoro katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Pia amempongeza Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi, kwa hatua ya kuwaleta pamoja viongozi wa kitaifa na watendaji wa vyama kwa lengo la kutoa elimu na kuimarisha msingi wa demokrasia.

“Tunakupongeza sana Msajili na ofisi yako kwa kazi nzuri ya ulezi wa vyama vya siasa. Umeona umuhimu wa kutukutanisha hapa ili kupitia Sheria ya Gharama za Uchaguzi, jambo hili ni jema kwa sababu linapunguza kasoro katika uchaguzi wetu,” amesema Khatibu.

Amesema awali baadhi ya vyama na wagombea walikuwa na uelewa mdogo walipotakiwa kuwasilisha taarifa za gharama za uchaguzi, jambo lililosababisha kuibuka kwa kasoro kubwa.

“Sheria hii ilipokuja mwaka 2010, watu wengi hawakuwa na uelewa. Wengine walijaza gharama za uchaguzi hewa wakidhani baada ya uchaguzi wangerejeshewa fedha. Watu walitengeneza risiti za kughushi, kumbe haipo hivyo. Hivyo basi leo tunatarajia kupata elimu ya kutosha,” amefafanua.

Khatibu amewataka viongozi na watendaji wa vyama kuchukua kwa umakini mkubwa mafunzo hayo ili, kuelekea Uchaguzi Mkuu, zoezi la kampeni na uchaguzi kwa ujumla liendeshwe kwa uwazi, uadilifu na kuepusha migogoro.

Nao baadhi ya washiriki kwenye mafunzo hayo wakiongea kwa nyakati tofauti wameomba ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kuitafsiri sheria hiyo kutoka lugha ya kiingereza na kuiweka kwenye lugha ya kiswahili ili iweze kueleweka kwa urahisi.

"Tunaomba fomu ziwe katika lugha ya kiswahili kwani wagombea wengi wanajua kusoma na kuandika kiswahili vizuri hivyo tunaomba waangalie namna ya kuweza kuibadilisha ili iweze kueleweka kwa watu wote",Amesema mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof,Ibrahim Lipumba.

Ameongeza pia Sheria ya gharama ya uchaguzi inamtaka  mgombea kuwa na akaunti binafsi jambo ambalo anaona halitawezekana kwa baadhi ya wagombea ambao wapo pembezoni mwa mji kwani huduma hiyo haipatikani.

Kwa upande wake Mgombea urais wa chama cha NLD Doyo Hassan amesema uwepo wa fomu zenye lugha ya kiingereza zinawatenga wagombea ambao awajui lugha hiyo badala yake watalazimika kujaza fomu hiyo chini ya usimamizi wa mtu mwingine au chama chake cha siasa.

KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI  MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA

KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.

TANZANIA KUWA KINARA WA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIMAABARA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

TANZANIA KUWA KINARA WA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIMAABARA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

MWENYEKITI CCM  RAIS  DKT.SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU.

MWENYEKITI CCM RAIS DKT.SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU.

WAANDISHI WA HABARI DODOMA WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA NA ULINZI.

WAANDISHI WA HABARI DODOMA WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA NA ULINZI.