

Mgombea Urais wa Chama cha United Democratic Party (UDP), Saum Hussen Rashid, pamoja na mgombea mwenza Juma Hamis Faki, wamechukua rasmi fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama hicho.
Dodoma. Mgombea Urais wa Chama cha United Democratic Party (UDP), Saum Hussen Rashid, pamoja na mgombea mwenza Juma Hamis Faki, wamechukua rasmi fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama hicho.
Fomu hizo zimekabidhiwa leo Agosti 14, 2025 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, katika hafla iliyofanyika makao makuu ya tume hiyo jijini Dodoma.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hizo, Saum ameishukuru INEC kwa mapokezi na utaratibu mzuri wa utoaji fomu, akibainisha kuwa chama chake kinaamini huu ni mwanzo wa uchaguzi huru na wa haki.
“Kama chama tumejipanga kuondoa changamoto zote kwenye jamii na kuwainua wananchi wanyonge, tunaamini Watanzania wanaweza kufanya maamuzi sahihi,” amesema.
Ameongeza kuwa vipaumbele vya UDP vinahusisha kuendelea kudumisha amani na utulivu vilivyoasisiwa na waasisi wa taifa, kutumia njia za amani kutatua migogoro, kuondoa ukatili wa kijinsia, na kuhakikisha rasilimali zote zinawanufaisha wananchi wote bila ubaguzi.
Kwa mujibu wa ratiba ya INEC, uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Rais na Makamu wa Rais unatarajiwa kufanyika Agosti 27, 2025.
WAZIRI MKUU AWATAKA TRAMPA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI KATIKA UTUNZAJI WA NYARAKA.
KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.
MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA
AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA
SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MGODI NYANDOLWA.
AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA
MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.
KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA