

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza wake Dkt.Emmanuel Nchimbi watachukua fomu za kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao.
Zoezi hilo litafanyika kesho, Agosti 9, 2025, katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla amesema kuwa hatua hiyo inaashiria kuanza rasmi kwa msimu wa kampeni za uchaguzi kwa vyama vyote vya siasa nchini.
"Baada ya kuchukua fomu, Mheshimiwa Rais atarejea Makao Makuu ya CCM hapa Dodoma, ambapo atapokelewa rasmi na viongozi pamoja na wanachama wa chama chetu, na kupata fursa ya kuwasalimia wananchi," amesema CPA Makalla.
Ameongeza kuwa, Dkt. Samia anagombea kwa awamu ya pili ya uongozi wake kwa mujibu wa Katiba, baada ya kumaliza kipindi cha kwanza cha miaka mitano, ambacho kitaisha rasmi mwaka huu.
Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, ambapo vyama mbalimbali vya siasa vitashiriki kikatiba kuwani nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani.
WAZIRI MKUU AWATAKA TRAMPA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI KATIKA UTUNZAJI WA NYARAKA.
KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.
MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA
AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA
AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA
SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MGODI NYANDOLWA.
MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.
WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA AFYA ZAO KWA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.