Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji Jacobs Mwambegele ametoa wito kwa wazalishaji wa maudhui mtandaoni kuzalisha maudhui yatakayo wahamisha wananchi kujitokeza katika kupiga kura kwa kuwa ni haki yao kikatiba na si kuweka maudhui yatakayohamasisha uvunjifu wa amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.

Wito huo ameutoa leo Agosti 3,2025 akifungua wakati wa mkutano wa Kitaifa wa Tume hiyo na wazalishaji wa maudhui mtandaoni kilichofanyima katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo amewataka waandaji hao kuandika habari za kweli zinasosimamia sheria kanuni na maadili.
"Hakikisheni taarifa zinazopandishwa katika kurasa zenu zinasimamia weledi ili kuepuka uvunjifu wa amani nchini Nawakumbusha juu ya umuhimu wa kuepuka matumizi mabaya ya akili unde ambayo inatumiwa na baadhi ya watu wenye nia ovu kusambaza habari za upotoshaji hasa kupitia mitandao ya kijamii," amesema.
Aidha ameongeza kuwa ni vema wazalishaji kutengeneza maudhui yatakayo wahamasisha vijana na watumiaji wa teknolojia kupitia mitandao ya kijamii kupata hamasa na kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi unatarajiwa kufanyika mnamo Oktoba mwaka huu.
Awali akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu na ushiriki wa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhan Kailima amesema Tume inatarajia vyombo vyahabari vitatumia kalamu zao na nyenzo walizonanzo kuhubiri amani katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi lakini pia kutoa nafasi sawa kwa wagombea wa vyama vyote katika vyombo vyao vya habari.
"Tume imejiwekea utaratibu wa kuvishirikisha vyombo vya habari katika mchakato mzima wa uendeshaji wa uchaguzi huu ili kuweka uwazi na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu, tunawaomba kutumia nafasi na fursa mlizonazo kuhakikisha kunakuwepo na taarifa za mara kwa mara za kuelezea kinachoendelea kuhusu uchaguzi, "Amesema Kailima
WAZIRI MKUU AWATAKA TRAMPA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI KATIKA UTUNZAJI WA NYARAKA.
KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.
MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA
AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA
SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MGODI NYANDOLWA.