

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa maono yake makubwa yaliyochangia kwa kiasi kikubwa kuifikia jamii ya vijijini kupitia upatikanaji wa nishati ya umeme na kuchochea kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.
Akizungumza katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Utawala wa REA, Bw. Renatus Msangira, alisema kuwa juhudi za Rais Samia zimewezesha kufikiwa kwa vijiji vyote nchini kupitia huduma ya umeme, na sasa wakala unaelekeza nguvu zake katika kusambaza huduma hiyo hadi kwenye vitongoji.
“Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi wa REA, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa maono yake. Kupitia dira yake, tumefanikisha kupeleka umeme katika vijiji vyote nchini, na sasa tumeanza awamu mpya ya kuhakikisha vitongoji vyote navyo vinaunganishwa na huduma hiyo muhimu,” alisema Msangira.
Aidha, alieleza kuwa REA inaunga mkono kwa vitendo kaulimbiu ya Rais Samia inayosisitiza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa afya na mazingira bora. Alisema wakala umeanza kusambaza majiko ya umeme yenye matumizi nafuu, likiwemo jiko linalotumia uniti moja tu ya umeme kwa saa moja.
“Hii ni sehemu ya kampeni ya matumizi ya nishati safi. Kwa sasa tumeanza na taasisi za umma, hasa zile zinazotoa huduma kwa watu zaidi ya 100, kama vile shule na hospitali, na tutaendelea kuwafikia wananchi wengine kote nchini,” alibainisha.
Bw. Msangira aliwataka wananchi kufika kwenye banda la REA katika viwanja vya maonesho Dodoma ili kujionea miradi inayotekelezwa na wakala huo, sambamba na kupata elimu kuhusu huduma za umeme vijijini na matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya umma kutoa huduma moja kwa moja kwa wananchi, kueleza majukumu yao na kutoa mrejesho wa maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya serikali.
Maiko Salali Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mpwapwa, Apongeza CCM kwa Ujumuishwaji wa Makundi Maalum
DIB YAHIMIZA WANANCHI KUDAI FIDIA ZAO KUTOKA BENKI ZILIZOFILISIKA
USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA
DWIGHT DANDA KIJANA MDOGO NA MHITIMU WA CHUO KIKUU ATIA NIA UBUNGE KIBAMBA
BoT YAWATAKA TAMFI NA TAMIU KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA.
Aliyeongoza kura maoni Vunjo 2020, kumkabili tena Dkt. Kimei
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake
Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma