

Nishati ya gesi asilia imekuwa na Mchango mkubwa Kwa nchi hasa kwenye Sekta ya umeme ambapo Serikali imewekeza kwenye bwawa la umeme hii ni nishati muhimu
Nasasa gesi hii ni muhimu Kwa Matumizi ya majumbani viwandani na magari nasasa upo mpango gesi hii itumike zaidi kwenye magari na maeneo mengine ya nchi Kwa gesi hiyo imekuwa ikipatika Mtwara Lindi na Dar es salam
Hayo yameelezwa Leo na Charles Nyangi Mkuu wa kitengo cha ushirikishwaji wa wazawa na ushirikishwaji wa ndani kutoka Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yaliyofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Ameongeza kuwa gesi hii itafika katika mikoa mingine kadri wananchi watakavyoielewa na kuona umuhimu wake Kwa kurahisisha na kuhimiza Matumizi ya nishati safi.
Aidha amesema Wapo kwenye Maonesho hayo kuwaelezea Wananchi kuhusu shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo pamoja na fursa zinazokuwepo katika shughuli za Mkondo wa juu wa Petroli
PURA ilianzishwa chini ya Sheria ya Petroli mwaka 2015 na moja la jukumu lilipoewa ni kuhamasisha ushiriki wa wawazawa katoka shughuli za Mkondo wa juu wa Petroli.
Amesema ushiriki huo umegawanywa katikati makundi matatu ambayo ni Kupitia ajira,kupitia ujasiriamali kwa maana ya kununua na kusambaza Bidhaa au uwekezaji.
" Hivyo tunapokuwa katika Maonesho haya ni kuwaelezea Wananchi majukumu na shughuli zinazopatikana kwenye mkono ," amesema
PURA ina matumaini kuwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, wawekezaji watakuwa wamepatikana, jambo ambalo litaleta manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Sanjari na hayo PURA inafanya kazi ya Kuwajengea uwezo watanzania na kampuni za Kitanzania kushiriki kikamilifu katika miradi ya utafutaji,uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia pamoja na kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za mafuta na gesi asilia nchini.
Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo "Himiza Matumizi ya mifumo ya kidijiti ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji"
Maiko Salali Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mpwapwa, Apongeza CCM kwa Ujumuishwaji wa Makundi Maalum
DIB YAHIMIZA WANANCHI KUDAI FIDIA ZAO KUTOKA BENKI ZILIZOFILISIKA
USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA
DWIGHT DANDA KIJANA MDOGO NA MHITIMU WA CHUO KIKUU ATIA NIA UBUNGE KIBAMBA
BoT YAWATAKA TAMFI NA TAMIU KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA.
Aliyeongoza kura maoni Vunjo 2020, kumkabili tena Dkt. Kimei
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake
Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma