

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba amesema kuwa katika miradi ya kimkakati inayotekelezwa nchini Wizara ya Nishati inatekeleza takribani miradi saba.
* Katibu Mkuu Nishati asema kati ya miradi hiyo saba, JNHPP imekamilika*
* Asema EACOP imefikia asilimia 65 huku Serikali ya Tanzania ikichangia hisa za shilingi trilioni 1.12*
*Ruhudji na Rumakali tafiti zakamilika*
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba amesema kuwa katika miradi ya kimkakati inayotekelezwa nchini Wizara ya Nishati inatekeleza takribani miradi saba.
Mhandisi Mramba ameyasema hayo Agosti 17, 2025 wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Vijana (YEE) ambao unagusa maeneo yanayopitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).
“Miradi hiyo ni mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), Mradi wa kugeuza gesi kuwa kimiminika (LNG), Mradi wa utafutaji mafuta, Miradi ya umeme ya Rumakali na Ruhudji na utafiti wa mafuta eneo la Mnazi Bay North”, amesema Mha. Mramba.
Ameeleza kuwa katika miradi hiyo saba, mradi wa bwawa la kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere unaozalisha megawati 2,115 umekamilika na unaingiza umeme kwenye gridi ya Taifa.
Ameongeza kuwa mradi wa bomba la mafuta ghafi (EACOP) umefikia asilimia 65 na upo mbioni kukamilika, mradi wa LNG upo katika hatua za mwisho na miradi ya umeme ya Ruhudji na Rumakali tafiti zimekamilika.
Aidha, amesema Serikali ya Tanzania imeshachangia takribani shilingi trilioni 1.12 kwenye mradi wa EACOP kama hisa ya Tanzania katika mradi huo na kuna kampuni za kitanzania 200 ambazo zinatekeleza kazi mbalimbali katika mradi wa EACOP ambazo zitalipwa i jumla ya shilingi trilioni 1.325.
Mhandisi Mramba ametanabaisha kuwa mbali ya fursa za kiuchumi zinazopatikana pia wananchi wa maeneo ambayo mradi ya umeme inayopeleka umeme EACOP itapita watanufaika kwa kuunganishwa na huduma ya umeme.
WAZIRI MKUU AWATAKA TRAMPA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI KATIKA UTUNZAJI WA NYARAKA.
KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.
MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA
AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA
AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA
SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MGODI NYANDOLWA.
MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.
WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA AFYA ZAO KWA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.