

Waziri wa viwanda na biashara Dk Suleiman Jaffo ametoa rai kwa wadau wote wa Serikali, sekta binafsi, na jamii kuungana katika kuweka mazingira yanayoruhusu ubunifu, uvumbuzi na kustawi kwa wabunifu nchini.
Waziri wa viwanda na biashara Dk Suleiman Jaffo ametoa rai kwa wadau wote wa Serikali, sekta binafsi, na jamii kuungana katika kuweka mazingira yanayoruhusu ubunifu, uvumbuzi na kustawi kwa wabunifu nchini.
Wito huo ameutoa leo Mei 21,2025 jijini Dar es salaam kwenye maadhimisho ya siku ya miliki ubunifu(IP)yaliyoandaliwa na Wakala wa usajili na biashara na leseni (BRELA)yakiwa na kauli mbiu isemayo 'Muziki na miliki ubunifu:sikiliza mdundo wa miliki bunifu'
Amesema Siku hii ni ukumbusho kwamba, muziki sio tu burudani, bali ni nguvu ya kubadilisha jamii, na utambuzi wa haki za miliki ubunifu ndizo zinazoiwezesha nguvu hiyo.
"Mimi kama Waziri mwenye dhamana na masuala ya Miliki Ubunifu, naahidi kuendelea kushirikiana na wadau wengine kupitia BRELA na COSOTA, kuimarisha ulinzi wa haki za Miliki Ubunifu nchini. Ninawasihi tuungane pamoja katika "kusikilizia mdundo wa miliki ubunifu" na kujenga mustakabali wa pamoja kuhakikisha wasanii na wabunifu wetu si tu wanalindwa na kuheshimiwa hapa nchini na nje ya nchi yetu, lakini pia wanapata manufaa kupitia bunifu zao."
Aidha amewataka wabunifu kubuni bunifu zinazolenga, kutatua Changamoto za kijamii, na kuhakikisha bunifu hizo zinalindwa na mwisho kuingizwa sokoni.
"Muziki wetu ni hazina ya kitaifa, na ni wajibu wetu kulinda wale wanaoupa uhai. Nawahimiza vijana wabunifu kuendelea kutunga nyimbo za burudisha na kuelimisha jamii. Serikali iko tayari kuwasaidia kupitia ruzuku na mikopo nafuu, mafunzo, na huduma za kisheria kupitia kwa BRELA, COSOTA na Taasisi nyingine",amesema.
Amesema Serikali, inaendelea kufanya mageuzi ya kisheria na kimifumo ili kuimarisha ulinzi wa haki za Miliki Ubunifu katika maeneo yote, ikiwa ni pamoja na kuwa na Sera ya Taifa ya Miliki Ubunifu; kuiboresha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki, Sheria ya Alama za Biashara na Huduma, Sheria ya Hataza pamoja na kuridhia mikataba mbalimbali ya kikanda na kimataifa ambayo inasimamia na kulinda hakimiliki na hakishiriki za wasani.
Sambamba na hayo Jaffo amewapongeza wasanii waliosajili alama zao huku akitoa rai kwa wasanii na wabunifu wengine kusajili alama zao kwa ajili ya kuzilinda.
"Nitatoa mifano michache ya wasanii waliotumia majina ya kisanii au nembo zilizotokana na kazi za muziki kufanya shughuli za kibiashara na kupata umaarufu sokoni. Nembo ijulikanayo kama shu shi by nandy (Faustina Charles Mfinanga almaarufu Nandy), African Boy (Juma Mussa Mkambala – Juma Jux), Chibu (Nasibu Abdul almaarufu Diamond Platnumz), Konde (Rajabu Ibrahimu Abdukahali – Harmonize), Kiba (Ally Salehe Kiba), na Mobetto style Boutique (Hamisa Said Mobeto)",amesema.
Kwa upande wake mtendaji mkuu wa wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA)amewataka Wasanii wa muziki nchini kusajili kazi zao na kuzilinda kupitia mifumo rasmi ya miliki bunifu ili kunufaika kiuchumi na kulinda kazi zao dhidi ya wizi wa ubunifu.
Aidha Nyaisa amesema licha ya muziki wa Tanzania kuvuka mipaka ya nchi, wasanii wengi bado hawajachukua hatua ya kusajili kazi zao, jambo linalowanyima fursa ya kunufaika na kazi hizo kisheria.
“Tunasisitiza muziki si burudani tu, ni biashara. Na biashara yoyote inalindwa. Wasanii wengi wanapoteza mapato kwa sababu kazi zao hazijasajiliwa,” amesema.
Nyaisa amesema BRELA imekuwa ikitoa elimu kwa wasanii kuhusu haki zao za ubunifu na kuwasogezea huduma ili waelewe namna bora ya kulinda kazi zao.
“Wapo wasanii wa zamani ambao nyimbo zao bado zinapigwa hadi leo lakini hawapati chochote kwa sababu hawakuzisajili. Hili ni pigo kwao na kwa familia zao,” amesema.
Ameongeza kuwa mabadiliko ya teknolojia yamekuwa na pande mbili; yamefungua fursa kwa wasanii lakini pia yameongeza changamoto ya matumizi holela ya kazi za muziki bila ridhaa ya wasanii.
BRELA imesema itaendelea kushirikiana na taasisi kama COSOTA ili kuhakikisha kazi za ubunifu zinalindwa na zinakuwa chanzo thabiti cha kipato.
Rais Samia Asisitiza Mchujo wa Wagombea Kufanyika Kwa Haki.
Ilani Ya CCM Imeandaliwa Kwa Weledi Mkubwa Kwa Kushirikiana Na Wananchi;RAIS Dkt.Samia
WIZARA YA ARDHI YAJA NA VIPAUMBELE SABA
SERIKALI NA WADAU WAENDELEZA MAPAMBANO YA KIJINSIA
KAPINGA ATAJA VIGEZO VYA ZIADA UPELEKAJI UMEME VITONGOJINI.
WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WAITWA JKT
WIZARA YA ARDHI YAJA NA VIPAUMBELE SABA
Ilani Ya CCM Imeandaliwa Kwa Weledi Mkubwa Kwa Kushirikiana Na Wananchi;RAIS Dkt.Samia
SERIKALI NA WADAU WAENDELEZA MAPAMBANO YA KIJINSIA
Rais Samia Asisitiza Mchujo wa Wagombea Kufanyika Kwa Haki.