

Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof.Elisante Ole Gabriel ametoa wito kwa wananchi wote pamoja na watumishi wa Ofisi yake mkoani Dodoma kujitokeza kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ili kuweza kupiga kura wakati wa uchaguzi ujao wa Serikali za Mtaa Novemba 27,2024.
Prof.Ole Gabriel amesema hayo Septemba 25,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuboresha taarifa zake kwenye daftari la kudumu la Mpiga kura katika kituo cha uandikishaji cha Damu Salama,Mtaa wa Tambukareli,kata ya Hazina.
Amesema kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imefanya vizuri katika zoezi hilo kwani mtu hana haja ya kwenda alikojiandikishia bali anaboresha taarifa zake alipo sasa na anapoweza kupiga kura na mifumo ya TEHAMA inamtambua hivyo imerahisisha kwa kila aliyefikia umri wa kupiga kura na tayari wenyevitambulisho vya mpiga kura kwenda kuboresha taarifa zao.
“Hili zoezi ni la kidigitali kwani mashine zinaweza kufanyakazi kwa mfumo wa betri hivyo hata sehemu ambazo hazina umeme zinaweza kufanyakazi.
“Lakini mimi nipo katika Mahakama na tunatumia mifumo ya TEHAMA na unaweza ukaingia kwenye mfumo ukaingiza taarifa zako halafu ukafika hapa ikawa rahisi zaidi kwasababu zitaonekana na hawa wenzetu wameweka namna ambayo mtu hawezi kujiboreshea mwenyewe moja kwa moja hadi afike kwenye vituo vya uandikishaki ili wasiweze kuruhusu wageni kujiandikisha,”amesema Prof.Ole Gabriel.
“Hivyo nitoe wito kwa wananchi wote wa Dodoma wajitokeze kwani zoezi ni la muda mfupi tu mimi nimetumia dakika tano na sekunde sita tu.
“Watumishi wenzangu wa Mahakama mjitokeze kuboresha taarifa zenu hii haisiani na dini wala Chama kwani kupiga kura ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu,”amesema.
Aidha ameongeza kuwa kwa sasa Tanzania inaenda vizuri kwenye suala zima la Tehama kwani ingemgharimu kutoka Dodoma hadi Dar es Salaam kuhakiki taarifa zake lakini tume imerahisisha ambapo yoyote anaweza kuhakiki taarifa zake pale alipo jambo ambalo ni zuri na litaokoa mda,na hii ni hatua nzurii kuona kama nchi kuna mahali pazuri tunaenda tofauti na tulipotoka
RC MAKALLA AWAHAKIKISHIA USALAMA WAZEE WA MKOA WA ARUSHA SIKU YA UPIGAJI KURA OKTOBA 29.
Mfalme wa Mashairi Awasha Moto wa Uzalendo: “Kura Yako Ni Silaha”
MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA KUWAKATAA WASIOHESHIMU MISINGI NA TUNU ZA NCHI
BRIGEDIA JENERALI NDAGALA AFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA USIMAMIZI WA MAAFA JIJINI MBEYA
Mkomi Awasisitiza Wakuu wa Taasisi Kusimamia Mifumo ya Kielektroniki Serikalini.
WAZEE WAASWA KUHAMASISHA JAMII KUJITOKEZA KUPIGA KURA.
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
TUMEJIANDAA VYEMA KUDHIBITI UHALIFU NA WAHALIFU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU- POLISI