Mavunde Kujenga Ulingo Wa Ngumi Jijini Dodoma | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

Mavunde Kujenga Ulingo Wa Ngumi Jijini Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde ameahidi kujenga ulingo wa ngumi kwa ajili ya mabondia wa Jijini Dodoma ikiwa ni hatua ya kuukuza na kuuendeleza mchezo wa masumbwi mkoani humo.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
22 Apr 2023
Mavunde Kujenga Ulingo Wa Ngumi Jijini Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde ameahidi kujenga ulingo wa ngumi kwa ajili ya mabondia wa Jijini Dodoma ikiwa ni hatua ya kuukuza na kuuendeleza mchezo wa masumbwi mkoani humo.

Mbunge Mavunde ameyasema hayo wakati alipomtembelea bondia Laurent Segu kutoka Dodoma ambaye atashiriki katika pambano la utangulizi dhidi ya Bondia Ibrahim Najum kutoka Mbeya ikiwa ni sehemu ya pambano la utangulizi kati ya Bondia Hassan Mwakinyo dhidi ya Bondia Kuvesa Katemba kutoka Congo pambano litakalofanyika Jijini Dodoma kesho Jumapili 23 April 2023.

“Nimekuja leo kukutembelea kambini kwako na nimeona maandalizi yako mazuri dhidi ya pambalo lililopo mbele yako, ni imani yangu utalinda heshima ya Dodoma na kufanya vizuri katika mchezo huu, Ushindi wako utakuwa ni kichocheo kikubwa kwa mabondia wengine wa Dodoma kufanya vizuri.

Mmekuwa na changamoto kubwa ya ulingo wa ngumi kwa muda mrefu, nataka kuwahakikishia kwamba mwaka huu nitawatengenezea ulingo  ili tuuendeleze huu mchezo wa masumbwi kwa kuwa na miundombinu mizuri na pia ili kuongeza hamasa ya mchezo huu ambao miaka ya nyuma ulileta heshima kubwa sana hapa mkoani Dodoma”Alisema Mavunde

Akitoa salamu za shukrani, Bondia Laurent Segu amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kusimamia mahitaji yake na kuwa karibu naye kipindi chote cha maandalizi ya pambano hili sambamba na motisha ya ushindi ya Tsh 1,000,000 na kuahidi kufanya vizuri katika pambano hilo ili kupeperusha vyema bendera ya Dodoma katika mchezo wa masumbwi.

TANESCO YAJA NA KAMPENI MAALUM YA KUHAMASISHA ULIPAJI WA MADENI KWA WATEJA.

TANESCO YAJA NA KAMPENI MAALUM YA KUHAMASISHA ULIPAJI WA MADENI KWA WATEJA.

ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 107 ZAKAMILISHA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI SIMIYU

ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 107 ZAKAMILISHA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI SIMIYU

MEATU MTAENDELEA KUPATA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO IKIWEMO NISHATI- DKT.SAMIA

MEATU MTAENDELEA KUPATA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO IKIWEMO NISHATI- DKT.SAMIA

Mifumo Ya Kidijitali Yaleta Mageuzi Makubwa Katika Sekta Ya Umma:Simbachawene

Mifumo Ya Kidijitali Yaleta Mageuzi Makubwa Katika Sekta Ya Umma:Simbachawene

BEI YA KUJAZA GESI (LPG) KWA MATUMIZI YA KUPIKIA NI HIMILIVU – KAPINGA.

BEI YA KUJAZA GESI (LPG) KWA MATUMIZI YA KUPIKIA NI HIMILIVU – KAPINGA.