

MAMLAKA ya uwekezaji na maeneo maalum Tanzania (TICEZA) imekuja na motisha ya kutoa maeneo bure kwa wawekezaji wazawa ambao wanataka kuanzisha Viwanda kwa lengo la kutoa ajira kwa Watanzania na kukuza pato la Taifa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo,Giliard Terry ameyaeleza hayo Agosti 6 katika Viwanja vya maonyesho ya Wakulima nanenane vilivyopo Nzuguni Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kongamano lilihosu masuala ya uwekezaji kwa wadau mbalimbali wakiwemo wakulima.
Terry amefafanua kuwa kukua kwa Miji nchini imekuwa inaleta fursa nyingi hasa katika biashara kwa wawekezaji wa ndani ambao wanataka kuwekeza katika Viwanda ambapo Serikali inataka kuwe na viwanda vya watanzania 100 ili kuhamasisha kila Mtanzania anayeweza kujiajiri katika kuelekea mageuzi ya Viwanda.
"Mheshimiwa Rais ametanua wigo wa fursa za kiuchumi kwa Watanzania wote wenye uwezo wa kuwekeza kwa kujenga Viwanda vya uzalishaji ambavyo watu watapata vipato vyao wenyewe kwa kutoa ajira kwa Vijana ambao hawana ajira.,"Amesema Mkurugenzi huyo
Aidha amebainisha kuwa mnamo Agosti 12,Mwaka 2025, saa 3 Asubuhi Jijini Dodoma,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Mipango na uwekezaji,Profesa Kitila Mkumbo atazindua huduma mpya za Mamlaka hiyo ambapo kuna maeneo matano maalum ,ikiwemo.Benjamin Mkapa lililopo Dar, Bagamoyo hekari 150 kwaajili ya viwanda,Dodoma hekari 680 ,eneo la Buzwagi na Kwala lililopo karibu na Mlandizi lenye hekari 100.
"Tutatangaza kuwa,kwa Mtanzania yeyote mwenye mtaji wa kuanzisha kiwanda na anania na ndoto ya kuwa na Kiwanda afike kwenye Mamlaka yetu atapewa eneo bure,tunataka watu wajitafutie vipato vyao wenyewe na kutakuwa na utaratibu wa mchujo kwa watakao jitokeza,"Amesisitiza Terry.
Sanjari na hayo,amebainisha kuwa wataweka utaratibu maalum wa mchujo ili kuondoa ujanjaujanja kwa wale ambao wadanganyifu ambao wanataka kumiliki maeneo tu lakini hawana uwezo wakumiliki kiwanda,lengo la Serikali ni kutaka watanzania wawe wanufaika namba moja katika nchi yao.
Kwa upande wake Charles Tulahi, muwakilishi msaidizi Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) amesema wanafanya kazi kwa ukaribu na Serikali ili kuhakikisha kunakuwa na uzalishaji bora,mazingira bora kwa kila mmoja.
Tulahi amesema kuwa mageuzi ya kilimo yanaweza kuondoa njaa ambapo wamekuwa na miradi ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ili kuhakikisha wanakuwa na maisha bora.
"Watanzania wawekeze kwenye Kilimo Kwa sababu kina tija kubwa kutokana na Kuongezeka Kwa Idadi ya watu na teknolojia"Amesema Tulahi
WAZIRI MKUU AWATAKA TRAMPA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI KATIKA UTUNZAJI WA NYARAKA.
KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.
MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA
AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA
AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA
SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MGODI NYANDOLWA.
MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.
WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA AFYA ZAO KWA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.