

Serikali imetenga kutoa zaidi ya shilingi bilioni 277 kila mwaka kwa ajili ya kugharamia huduma mbalimbali za Virusi Vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI nchini, ikiwa ni hatua ya kupunguza utegemezi wa wafadhili wa kimataifa katika mapambano dhidi ya janga hilo.
Hayo yameelezwa Agosti 6, 2025 na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Samwel Sumba, alipokuwa akizungumza katika Maonesho ya 32 ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, alipotembelea mabanda ya Ofisi ya Waziri Mkuu, yakiwemo mabanda ya TACAIDS.
Dkt. Sumba amesema kuwa uwekezaji huo mkubwa wa Serikali unaonesha dhamira ya dhati ya kuimarisha afua za VVU na UKIMWI kwa kutumia rasilimali za ndani, hatua ambayo inalenga kudhibiti kwa ufanisi zaidi maambukizi mapya na kuboresha maisha ya watu wanaoishi na virusi hivyo.
"Ni muhimu kwa nchi kuanza kujitegemea kifedha katika mapambano haya, hii itasaidia kuhakikisha huduma zinaendelea kupatikana kwa uhakika na kwa wakati, hata kama misaada kutoka kwa wafadhili itapungua au kusimama," amesema Dkt. Sumba.
Aidha, ameeleza kuwa kwa mujibu wa ripoti ya Utafiti wa Athari za UKIMWI ya mwaka 2022/2023, Tanzania inakadiriwa kuwa na watu wanaoishi na VVU kati ya 1,540,000 hadi 1,700,000 huku Kiwango cha maambukizi kwa watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi kimefikia asilimia 4.4, ambapo wanawake wanaongoza kwa asilimia 5.6 ikilinganishwa na wanaume wenye asilimia 3.0.
Hata hivyo, Dkt. Sumba ameongeza kuwa pamoja na takwimu hizo, bado kuna mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha zaidi ya miaka ishirini iliyopita.
"Iwapo tutalinganisha hali ya sasa na miaka ya 2000, tumeona kupungua kwa kiwango cha maambukizi, vifo na unyanyapaa. Hili ni jambo la kupongezwa," amesisitiza .
Maonesho ya Nanenane mwaka huu yameendelea kuwa jukwaa muhimu si tu kwa sekta ya kilimo na mifugo, bali pia kwa taasisi mbalimbali za kijamii na kiafya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya msingi ya maendeleo ya binadamu, ikiwemo afya ya jamii.
WAZIRI MKUU AWATAKA TRAMPA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI KATIKA UTUNZAJI WA NYARAKA.
KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.
MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA
AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA
AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA
SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MGODI NYANDOLWA.
MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.
WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA AFYA ZAO KWA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.