Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ubungo imewataka viongozi wa dini na washirika wao kutafuta suluhu ya migogoro inayojitokeza ndani au nje ya Makanisa au Misikiti ili kudumisha misingi ya amani na umoja katika taasisi zao za dini.

Akizungumza na viongozi wa dini wa Kanisa la wasabato Kwembe na Magomeni katika kikao chao cha kutafuta suluhu ya mgogoro wa ardhi wa kanisa la Waadventist Kwembe Kibamba jijini Dar es salam Katibu Tawala wa wilaya Ubungo(DAS) Hassan Mkwawa amesema kuwa viongozi wa dini ni mfano bora kwa upande wa serikali na raia wanaowazunguka hivyo wana wajibu wa kudumisha umoja na utulivu na kusisitiza kuwa endapo itatokea changamoto basi wana wajibu wa kumaliza changamoto zao pasipo kuzitoa hadharani.
"Ninawataka viongozi wa kanisa hili kuzingatia misingi ya mafundisho ya imani zao Ili kuimarisha na kudumisha amani pasipo kuweka taharuki ya changamoto zao kwani jamii inazimini Taasis za hizi kama majibu maswali yao",alisema Ndugu Mkwawa.
Katika hatua nyingine aliyekuwa Mjumbe wa Selikali ya kijiji cha Kwembe 1992 na Muumuini wa kanisa hilo la Waadventist(Wasabato) Bw.Joshua Hamathe akithibitisha kuwa Serikali ya kijiji cha Kwembe ilitoa maeneo ya kuabudia kwa kila dhehebu wakiwemo na wao na wakaendelea na Ibada zao lakini kinachomshangaza ni jinsi viongozi wa Kanisa la Magomeni walivyowazunguka kuhusu eneo hilo la ibada walilokabidhiwa.
Hamathe akaongeza kuwa, "Nina historia nzuri juu ya eneo hili hivyo wito wangu kwa Kanisa ni kwamba tunalichafua kanisa kwa sababu nilitegemea sisi ni watu wa kiroho kwamba utatuzi wake ungekuwa rahisi zaidi na wangelirudisha eneo tulilopewa,pia ninaiomba serikali ifanye utatuzi kuhusu changamoto hii".
Kwa upande viongozi wa Magomeni Mch.Emmanuel Andrew na Mwenyekiti wa jimbo dogo Pwani ya Mashariki amesema wanasubiri suluhisho litakalofanywa na serikali tutakapokutana tena kwenye kikao kijacho.
WAZIRI MKUU AWATAKA TRAMPA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI KATIKA UTUNZAJI WA NYARAKA.
KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.
MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA
AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA
AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA
SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MGODI NYANDOLWA.
MRADI WA TACTIC KUBADILISHA MANDHARI YA JIJI LA DODOMA
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.
WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA AFYA ZAO KWA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.